Dodoma/Zanzibar.
Wabunge mashabiki wa klabu ya Simba wanaoshiriki vikao vya Bunge
vinavyoendelea jijini Dodoma, jana walifanya kikao Msalato, nje kidogo
ya mji lengo likiwa ni kupanga mikakati ya kuhakikisha timu inapata
ushindi kwenye mechi ya kufunga msimu dhidi ya Yanga Jumamosi wiki hii
kwenye Uwanja wa Taifa.Timu hizo
zinakutana kufunga msimu, huku Yanga ikiwa tayari imeshatawazwa ubingwa
kabla hata ya mechi kumalizika na Simba ikijihakikishia nafasi ya tatu
kutegemea matokeo ya mchezo huo.Juzi
jioni Naibu Spika Job Ndugai, alitangaza bungeni wakati akisoma ujumbe
wa maandishi wa Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani,
aliouandika akitaka Ndugai kuwatangazia wabunge wanaoishabikia timu hiyo
kukutana.“Kuna mambo muhimu
sana lazima niyatangaze sasa hivi, Mheshimiwa Ngonyani anawatangazia
wabunge wote mashabiki wa Simba kesho (jana) wakutane kule wanakokutana
Msalato kwa ajili ya kupanga mikakati,” alisema Ndugai.“Hapa
nimekaa na mwenyekiti wa Simba, Aden Rage na yeye kaniambia wale wote
(Waziri wa Ujenzi John Magufuli) na Naibu wake (Gerson Lwenge) ni Simba
pia,” alisema Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba (CCM) wakati
akichangia hotuba ya Wizara ya Ujenzi.
Juzi,
Mbunge wa Urambo Magharibi, Juma Kapuya, alimshauri Mwenyekiti wa Klabu
ya Simba, Ismail Aden Rage kuwataka yosso wa Simba kuwafunga ‘babu’ zao
wa Yanga.
Wabunge
mashabiki wa Simba ni Rage (Mwenyekiti wa Simba), Ndugai (Kongwa),
Ngonyani, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta
(Urambo Mashariki), Kapuya, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe
(Chadema).
Idd Azzan
(Kinondoni), Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Amos Makala
(Mvomero), Murtaza Mangungu (Kilwa Kaskazini) Naibu Waziri wa Ujenzi,
Gerson Lwenge, ( Njombe Magharibi), Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na
Ushirika, Adam Malima, (Mkuranga) na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli.
Wakati
huohuo, mashabiki wa Simba wametakiwa wasiwe na hofu na wajazane
uwanjani kuona timu yao ikiwaadhiri watani wao wa jadi, Yanga.
Kocha
Mkuu wa Simba, Patrick Liewig na msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’
walitamba jana mjini Zanziba kuwa Simba iko imara na itaibwaga Yanga.
Mwananchi