Tukio
la kutupwa bomu katika Kanisa Katoliki la Joseph Mfanyakazi, Arusha
limetua katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) baada ya
kuwasilishwa na Balozi wa Vatican UN, Askofu Mkuu Frances Chullikatt.
Askofu
Chullikatt anakuwa kiongozi wa kwanza wa Vatican kutoa tamko kuhusiana
na shambulizi hilo ambalo mmoja wa viongozi wake alikuwapo.
Bomu
hilo lilirushwa katika kanisa hilo wakati likizinduliwa na Balozi wa
Vatican nchini, Askofu Mkuu Francisco Padilla Mei 5, mwaka huu na
kusababisha vifo vya watu watatu na
kujeruhi zaidi ya 50.
kujeruhi zaidi ya 50.
Wakati wa shambulizi hilo, Askofu Padilla na Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha, Josephat Lebulu walionusurika.
Akihutubia
Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, New York, Marekani
juzi, Askofu Chullikatt alisema tukio lililotokea Arusha linadhihirisha
kuwa kuna umuhimu ya kupambana na ugaidi katika Afrika ili kuimarisha
amani na usalama wa kimataifa.
“Unahitajika
mshikamano na ushirikiano wa pamoja wa mataifa mbalimbali katika
kuchukua hatua za maisha na kulinda haki za binadamu,” alisema Askofu
Chullikatt, ambaye amekuwa mwakilishi wa Vatican kwenye Umoja wa Mataifa
tangu mwaka 2010.
Askofu
Chullikatt, ambaye ni mzaliwa wa India, alisema suala la ugaidi
linahitaji kuzuiwa duniani kote na hasa Afrika kutokana na matukio hayo
kuharibu maisha ya binadamu na kutokea katika maeneo wanayofanyia ibada.
Askofu
Chullikatt alisema pale ugaidi unapofanyika kwa kutumia dini, waumini
na viongozi wao ni lazima wahakikishe wanapambana nao ili kuutokomeza.
Alisema
suala la ugaidi linahitaji viongozi wa kisiasa, kijamii na kidini
kulilaani kwani ni la kikatili katika maisha ya binadamu hivyo si vyema
kukaa kimya suala hilo linapotokea.
Askofu
Chullikatt alisema ugaidi unaotokea Afrika unatakiwa kuangaliwa
kimataifa ili kuzipa uwezo nchi hizo kupambana na kuzuia matukio hayo.
Shambulio la bomu dhidi ya kanisa la Arusha lilikuwa tukio la pili la ugaidi uliolenga kushambulia wageni nchini.
SOURCE::MWANANCHI:::
SOURCE::MWANANCHI:::