Shirikisho la soka Tunisia TFF linatarajia kupeleka maombi ya kuandaa kombe la dunia la vijana mwaka 2017 la U20 .
Uamuzi huo umekuja baada ya kamati ya utendaji ya chama hicho uliofanyika jijini TUNIS siku ya jumanne.
Taifa hilo la afrika ya kaskazini linataka kuandaa mashindano hayo kwa mara ya pili baada ya kuandaa kwa mara ya kwanza mwaka 1977.
Kombe la dunia la vijana linatarajia kuanza mwaka huu wa 2013 ambalo litafanyika mwaka nchini Uturuki mwaka kuanzia June 21 na July 13, huku Egypt, Ghana, Mali na Nigeria zikiiwakilisha Africa.