Mwanamke
- anayejiita Sister Phylis Wanjiru Kamau, raia wa Kitui nchini Kenya
akiwa ofisi za kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa, baada ya
kukamatwa
Taarifa za kipolisi, za kukamatwa kwa Sister Feki Phylis Wanjiru Kamau.
JESHI
la polisi mkoa wa Iringa limemkamata mwanamke Phylis Wanjiru mwenye
umri wa miaka 44 aliyevalia mavazi ya kitawa wa masister wa kanisa
Kathoriki, ambapo baada ya kupekuliwa amekutwa na baadhi ya vielelezo
vilivyobaini kuwa ni tapeli.
Wanjiru ambaye ni raia wa nchi ya Kenya
amekamatwa na jeshi la polisi baada ya masister wenzie kubaini kama si
mmoja wao, kutokana na kushindwa kufanya baadhi ya masuala ambayo ni
msingi wa utawa wao.
Akizungumzia mkasa huo, kamanda wa
jeshi la Polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda amesema mwanamke huyo
kabila laKe ni Muwembu wa nchini Kenya amekamatwa katika nyumba za
masista zilizopo Ipogolo mjini Iringa.
Aidha Kamuhanda amesema mwanamke
huyo ambaye awali aligoma kutoa maelezo ya kina juu ya ujio wake nchini
Tanzania, katika upekuzi walimkuta na baadhi ya chip (Line) za makampuni
mbalimbali ya simu ya ndani na nje ya nchi.
Kamuhanda amesema Sister huyo bandia
alikutwa pia akiwa na hati za kusafiria (Passport) mbili, moja ikiwa
niya Africa Mashariki yenye namba Ke. 020659 huku hati ya nyingine ikiwa
na jumuiya ya Kenya namba A. 1790366.
Amesema Sister huyo feki katika hati
hizo ilionyesha kuwa alitembelea nchi ya Rwanda, Uganda pamoja na
nchini Tanzania ambapo siku za hivi karibuni alikuwa Mkoani Mara Tarime.
Sister huyo FEKI amekuwa akitumia
mbinu ya kujiangusha kama mtu mwenye ugonjwa wa kifafa pindi
anapofanyiwa mahojiano, jambo linalowawia vigumu jeshi hilo kupata
maelezo ya kina dhidi ya dhamira yake ya kuingia humu nchini.
Kamuhanda ameitaka jamii kuwa makini
na wageni mbalimbali, huku akiwaasa kuacha tabia ya kuwaamini watu kwa
muonekano wao, kutokana na mwanamke huyo kutumia njia hiyo ambayo
inamfanya kila mtu kumuamini.
>>>>>>Katika tukio
lingine jeshi la Polisi mkoani hapa linamshikiria mtumishi wa Mahakama
ya Wilaya ya Iringa kwa tuhuma za kuiba vielelezo vya madawa ya kulevya
aina ya bangi.
Kamuhanda
amesema tukio hilo limefanyika tarehe 14 ambapo mtuhumiwa huyo wa
mahakama Lwitiko Lusekelo Minga ambaye ni mlinzi wa Mahakama ya Wilaya
ya Iringa, aliiba bangi yenye uzito wa kg 371.2
“Tukio la kupatikana kwa bangi, eneo la
Flerimo mtuhumiwa Juma Nzowa alikamatwa na bangi na baada ya kuhojiwa
mtuhumiwa alimtaja Lwitiko Lusekelo Minga Mlinzi wa Mahakama kuwa ndiye
aliyemuuzia kielelezo hicho cha mahakama,” Alisema Kamuhanda.
Pia amesema kielelezo hicho awali kilikamatwa Wilaya ya Kilolo na kufikishwa mahakamani kama ushahidi na ndipo ilipoibiwa tena.
Amesema kutokana na uwepo wa
watumishi wasio waaminifu kumekuwa na tabia hiyo hasa kwa madawa hayo ya
kulevya, vielelezo vyake na kurudi tena mitaani huku wao wakiendelea na
zoezi la kukamata.
Hata hivyo kumekuwa na malalamiko
mbalimbali juu ya vielelezo hivyo kuibiwa pindi vifikapo Mahakamani,
hasa kwa vidhibiti hivyo vya madawa ya kulevya na vipodozi mbalimbali
ambapo huuzwa katika maduka na wananchi kuendelea kutumia.
Aidha vielelezo kama vyombo vya thamani navyo vimesemekana mara nyingi hupotelea Mahakamani na hata katika vituo vya Polisi.
Habari na :Oliver Motto- Iringa
Mwanamke -
anayejiita Sister Phylis Wanjiru Kamau, raia wa Kitui nchini Kenya
akiwa ofisi za kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa, baada ya
kukamatwa.