Mwenyekiti
wa Chama cha CUF, Mheshimiwa Profesa Ibrahim Lipumba amekaririwa na
Gazeti la Mwananchi la leo, Jumatano, Mei 15, 2013 akisema kuwa “amenasa
taarifa za siri za kuwepo kwa mipango ya kuongeza muda wa Serikali ya
sasa kukaa madarakani”.
Katika
habari hiyo iliyoandikwa chini ya kichwa cha habari,“Lipumba: Kuna
njama za kumwongezea JK muda”Mheshimiwa Lipumba anadai kuwa Serikali ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete “ itakaa madarakani hadi mwaka 2017” kwa sababu kuna“wasiwasi
kuwa mchakato wa sasa wa kupata Katiba Mpya hautaweza kukamilika mwaka
2014.”
Taarifa
hiyo imedokeza kuwa itakuwa ni vyema kwa Mheshimiwa Lipumba kuisaidia
jamii kusema nani anafanya mpango huo ili ukweli ujulikane.
Aidha,
Mheshimiwa Rais anawasihi wanasiasa na Watanzania kwa ujumla kuacha
tabia za uongo na uzushi na kuwapotezea muda Watanzania kufikiria mambo
yasiyokuwepo.
Ukweli
ni kwamba, kama ambavyo amesema mara nyingi, ni matarajio ya Rais
Kikwete kuwa mchakato wa Katiba utakamilika mwaka 2014 na kuwezesha
Uchaguzi Mkuu wa 2015 kufanyika chini ya Katiba Mpya kama inavyotarajiwa
na kumpa nafasi ya kustaafu mwisho wa kipindi chake cha uongozi wa
taifa letu.