Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Thursday, May 30, 2013

SETH APAMBANA KUINUSURU KANUMBA THE GREAT FILM ISIFE


Seth Bosco.
 
 
 MDOGO wa aliyekuwa mwigizaji maarufu wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Seth Bosco amefunguka kuwa anafanya kazi kwa bidii ili kuinusuru Kampuni ya The Great Film aliyoiacha marehemu kaka yake isife.
 
 
Akichezesha taya na paparazi wetu, juzikati jijini Dar, Seth alisema kutokana na pengo kubwa aliloliacha Kanumba, anajaribu kufanya kazi kwa bidii za kuaandaa filamu mpya ambazo wanawashirikisha wasanii tofauti wa Bongo ili kuinusuru kampuni hiyo.
“Yaani nafanya kazi kwa bidii sana kwa kushirikiana na wafanyakazi wa kampuni aliyoiacha Kanumba, japokuwa hatuwezi kufanya vizuri kama alivyokuwepo mwenyewe lakini tunaamini kujitahidi kwetu kutasaidia,” alisema Seth.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...