Mama Mzazi wa msanii Albert Kenneth Mangwair, Bi Denisia Mangwair akiwa na simanzi msibani leo.Dada wa marehemu, Magreth Mangwair, naye akiwa na majonzi ya kuondokewa na kaka yake.
NI simanzi na majonzi kutoka nyumbani kwa Mama Mzazi wa msanii Albert
Kenneth Mangwair, Bi Denisia Mangwair (63) maeneo ya Kihonda ‘Mazimbu
Road’ mkoani Morogoro ulipo msiba wa msanii huyo. Msibani hapo pia
alikuwepo dada yake marehemu, Magreth Mangwair ambaye alikuwa na majonzi
kwa kuondokewa na kaka yake mpendwa.
(PICHA ZOTE NA DUSTAN SHEKIDELE / GPL, MOROGORO)