Wauguze
wa mkoa wa morogoro wakiwa kwenye maandamano na hapa wanaingia kwenye
viwanja vya manispaa ya morogoro katika siku ya wauguzi.
MKUU
wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera asubuhi ya leo amepokea maandamano ya
wauguzi wa mkoa wa Morogoro ambao waliungana na waunguzi wote duniani
kuadhimisha siku ya waunguzi inayoadhimishwa kila mwaka mei 12.
Lengo
kuu la kuadhimisha siku hiyo ni kumuenzi muasisi wa wauguzi duniani
ndugu Florance Nightingale ambapo kwa wauguzi wa Morogoro waliadhimisha
siku hiyo kwa kuandamana na maandamano hayo kupokewa na mkuu wa mkoa wa
Morogoro kwenye ukumbi wa Manispaa ya Morogoro.
Mkuu
wa mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera wa tatu kutoka kushoto akiwa na
viongozi wa wauguzi wa mkoa wa morogoro na viongozi wandamizi wa mkoa
huo wa idara ya afya.
Wauguzi wakiburudika wakati wa siku ya wauguzi.