Rais Xi Jinping wa China amekutana na askofu mkuu wa Russia wa dhehebu la Orthodox Patirarch Kirill leo hapa Beijing. Rais Xi amesema urafiki mkubwa wa jadi na mahitaji halisi yamewaunganisha watu wa China na Russia, anatarajia kanisa la Orthodox la Russia na askofu mkuu Kirill watatoa mchango mkubwa zaidi katika kusukuma mbele urafiki kati ya nchi hizo mbili.
Rais Xi pia amelishukuru kanisa la Orthodox la Russia kwa kushikilia kuunga mkono maendeleo ya uhusiano kati ya China na Russia, na kuiunga mkono China katika masuala makubwa yakiwemo mamlaka, usalama, ukamilifu wa ardhi na maendeleo ya China.
Katika ziara yake ya siku 6 hapa China, askofu mkuu Kirill atatembelea miji ya Beijing, Shanghai na Harbin.