Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Friday, May 17, 2013

POLISI YAWATIA MBARONI KANGAMOKO ..... RIPOTI KAMILI HII HAPA

JESHI la Polisi Mkoa wa Kinondoni, linalishikilia baadhi ya wanenguaji wa kundi maarufu kwa kucheza maungo yakiwa wazi ‘Kanga Moko na Laki si Pesa’, gazeti la Tanzania Daima la leo lina hatimiliki ya hii habari.
Watuhumiwa hao wamekamatwa sambamba na watu wengi wanaofanya biashara ya kuuza miili yao, kufanya mapenzi hadharani na vitendo vya kishoga.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema kuwa kundi hilo sambamba na watu hao walikamatwa katika maeneo ya Hoteli ya Travertine, Ambiance Club, Kinondoni Makaburini, endelea kupitia na kukopi  audifacejackson blog.Coco Beach na Barabara ya Tunisia.“Tumewakamata hao wanaofanya mchezo maarufu wa Kangamoko na Laki si Pesa na tayari wanafikishwa mahakamani muda wowote na msako bado unaendelea ili kudhibiti vitendo hivyo na michezo hiyo ya kangamoko au baikoko ambayo watu wengi wameilalamikia kutokana na mtindo wanaoutumia,” alisema.
Kundi la kangamoko limekuwa likilalamikiwa mara kwa mara kutokana na kucheza wakionesha maungo ya miili yao wazi na kuvaa nguo nyepesi wanazozimwagia maji.
Kukamatwa wasanii wa kundi hilo kumekuja siku chache tu tangu walalamikiwe katika Bunge la Jamhuri ya Muungano kwamba wamekuwa wakipotosha jamnii.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...