Obama asema atafanya majaribio mengine ya kulifunga gereza la Guantanamo Bay
Rais Barack Obama wa Marekani ametangaza kuwa, atafanya majaribio
mengine ili kufunga gereza la Guantanamo Bay ambalo watuhumiwa wenye
msimamo mkali wa kidini wanashikiliwa.
Obama amesema amepeleka tume ya maofisa kushughulikia suala hilo, na atalifikisha tena suala hilo mbele ya bunge.
Hata hivyo Obama hajapata njia mpya ya kuondoa vizuizi bungeni dhidi ya juhudi zake za kufunga jela hiyo.