Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Friday, May 3, 2013

Majeshi ya Umoja wa Afrika yazuia njama ya shambulizi la kigaidi katika bandari ya Kismayu

Kikosi cha tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM kimesema kimevunja jaribio la mashambulizi mawili yaliyopangwa kufanywa wiki hii na magaidi wanaodhaniwa kutoka kundi la Al shabaab dhidi ya bandari ya Kismayu. 

Kamanda wa kikosi cha AMOSOM Bw Andrew Gutti ametoa taarifa akisema, majeshi ya AMISOM yalimkamata mwanamke aliyekuwa na mabomu akijaribu kuingia katika Chuo Kikuu cha Kismayu, ambako wajumbe walikuwa wanakutana kujadili mchakato wa kisiasa wa Jubaland. 

Majeshi hayo pia yamezuia jaribio lingine la shambulizi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kismayu. 

Bw Gutti amesema kundi moja la watu waliokuwa wanapanga kufanya shambulizi kwenye uwanja wa ndege liligunduliwa na wanajeshi wa AMISOM na kupambana nao.

 Magaidi hao waliwashambulia wanajeshi wa AMISOM kwa mizinga, baadhi ya mizinga iliangukia karibu na uwanja wa ndege, na magaidi hao walikimbia.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...