Wakati Rais wa Marekani, Barrack Obama akitarajiwa kuwasili na msafara
wa watu 700, baadhi ya hoteli zenye hadhi ya nyota tano jijini Dar es
Salaam zimeanza kusitisha kupokea wageni kutokana na ujio huo.
Taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani ilisema Rais huyo,
anatarajiwa kuwasili nchini Julai Mosi kwa ajili ya ziara ya siku tatu
hadi Julai 3 mwaka huu ili kuimarisha uhusiano baina ya nchi hiyo pamoja
na nchi za Afrika. Msafara huo utajumuisha watu mbalimbali wakiwamo
wafanyabiashara.




