Kutoka
kushoto ni John Tegete baba mzazi wa mchezaji nyota wa yanga Jerry
Tegete,kulia ni Kalfan Ngassa baba mzazi wa mchezaji nyota wa Simba
Mrisho Ngassa,wakihojiwa na mtandao huu ndani ya uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza jumamosi iliyopita.Mrisho
ni mtoto wa Khalfani Ngassa aliyewahi kung'ara na timu ya Pamba ya
Mwanza na Simba huku Mzee Tegete pia aliwa kuwa mchezaji tegemeo wa
Pamba wakati watoto zao wakingara kwenye timu kubwa za simba na yanga
wazee hao wanaendeleza fani hii ya Soka ambapo mzee Tegete mbali ya kuwa
meneja wa uwanja wa CCM Kirumba pia ni kocha mkuu wa timu ya Toto
Afrika iliyoshuka daraja msimu huu huku Mzee Ngassa akipewa jukumu la
ukocha mkuu timu ya Polisi lringa inayoshiriki ligi daraja la kwanza.
Juzi
jumamosi Mtandao huu uliwafuma wazee hao wakibadilishana mawazo huku
wakiwa na furaha na afya njema wakiendela kula matunda ya watoto wao
ambao mbali ya kuwa tegemo kwa timu zao pia ni wachezaji muhimu kwa timu
ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars.kwa sasa.
Kwa pamoja walipohojiwa na mwandishi
wa habari hizi kuhusiana na maendela ya watoto wao wazee hao walidai
kwamba kila kukicha wanawaasa watoto zaokufanya mazoezi kwa bidii na
kuepukana na mambo ya anafa ambayo.
Kutoka
kulini ni Juma Amir,kati John Tegete na kulia ni Khalfani Ngassa wakiwa
kwenye picha ya pamoja baada ya kuhojiwa na matanda huu.



