Charles Mullinda
Mhariri Mtanzania Jumatano
Kaimu Mwenyekiti
Jukwaa la WahaririYAH: KUJITOA KWENYE
JUKWAANapenda kukufahamisha kuwa nimeamua kujitoa kwenye Jukwaa la
Wahariri kwa sababu siridhiki na mwenendo wa Jukwaa hilo.Nimeamua
kujitoa kwa sababu sijaridhishwa na uamuzi uliofikiwa wa kuingilia uhuru
wa habari na kufumbia macho baadhi ya mambo ambayo ninaamini
hayapaswi kufumbiwa macho.
Uamuzi wangu huu pia unatokana na jinsi jukwaa linavyotumia nguvu kubwa kuficha ukweli unao wahusisha
baadhi
ya wahariri ambao gazeti hili lilibaini kuwa walikuwa na mawasiliano
yenye utata na aliyekuwa mtuhumiwa wa ugaidi, Joseph Ludovick.Aidha,
siridhishwi na jinsi baadhi ya wahariri wanavyoshambuliwa na wahariri
wenzao katika magazeti yao pasipo Jukwaa kuchukua hatua huku kwa upande
mwingine likitumia nguvu kubwa na pesa nyingi kuwalinda baadhi ya
wahariri ambao nyendo zao zinatia mashaka.
Kikao
cha kwanza na TEF na kilichofanyika leo kimedhihirisha pasipo mashaka
kuwa TEF iliamua kuwa na ajenda maalumu ya kumshughulikia Mullinda kwa
kuwa tu nilionyesha mawasiliano ya Deodatus Balile na Ansbert Ngurumo
dhidi ya Ludovick kama ambavyo gazeti la Tanzania Daima lilivyoonyesha
mawasiliano ya Dennis Msaki na Ludovick..
Ripoti
ya timu iliyoundwa kuchunguza ukweli wa habari iliyoandikwa na gazeti
la Mtanzania Jumatano ina upungufu mkubwa wa kimantiki ambao hata kwenye
kikao niliuonyesha lakini haukusikilizwa.Ushahidi wa Ngurumo kumtuma
pesa Ludovick upo wazi, lakini hakuna mtu anayeliangalia hilo kwa sababu
tu timu ile iliundwa kumshughulikia Mullinda kwa sababu aliandika
vigogo wa TEF ambao wako karibu na viongozi wa TEF.
Nimeamua kujitoa baada ya kubaini kuwa jukwaa linafanya kazi kwa ajili ya maslahi ya watu binafsi.
Kwa taarifa hii naamini utaratibu wa kawaida wa kuagana utazingatiwa.Charles Mullinda.