![]() |
| Kanhaiya Kumari (kushoto) akiwa na mama yake, Vijaya mara baada ya kuachiwa huyu. |
Mtoto mdogo
wa kiume wa mwanamke ambaye amedhoofika kwenye jela kwa takribani miaka
20 nchini India kwa upungufu wa Pauni za Uingereza 119
katika pesa za dhamana hatimaye amehakikisha kuachiliwa huru kwa mama yake.
Kanhaiya Kumari, mwenye umri wa miaka 19, alizaliwa ndani ya gereza
na Vijaya, mwenye miaka 48, ambaye alikamatwa mwaka 1993 kwa kuhusiana
na kesi inayohusisha mauaji ya mmoja wa majirani zake katika wilaya ya
Aligarh nchini India.
Alipatiwa dhamana mwaka 1994 lakini - ilitupwa na mumewe - hakuwa na
uwezo wa kulipa Rupia 10,000 iliyokuwa ikihitajika kuhakikisha uhuru
wake. Sasa ameungana tena na mtoto wake wa kiume, baada ya mtoto huyo
kuwa amefanya kazi kupata pesa hizo za dhamana na kuishawishi Mahakama
Kuu kwa ajili ya kuachiliwa mama yake.
Kanhaiya alikana kuhusika kwa namna yoyote katika kesi hiyo ya kihistoria ya mauaji kwenye kijiji cha Mahrauni mjini Aligarh.
Alikamatwa huku akiwa na ujauzito wa miezi mitano, akajifungua mtoto
Kanhaiya huku akiwa amefungwa jela, ambapo baadaye mama na mtoto
walipelekwa katika gereza la Nari Niketan lililoko Lucknow, Uttar
Pradesh.
Vijaya alipewa dhamana na mahakama mwaka 1994, lakini mumewe aligoma kutuma pesa za dhamana kiasi cha Rupia 10,000.
Kanhaiya alipelekwa kwenye jela ya watoto mjini Lucknow akiwa na umri
wa miaka 11, ambapo alitumikia miaka 7 kabla ya kuachiwa huru mwaka
jana.
Mapema tangu kuruhusiwa kutoka kwenye jela hiyo, Kanhaiya akapata
kazi katika kiwanda kimoja na kujipanga kukusanya kiasi cha pesa za
dhamana ili kumwezesha mama yake kuachiwa huru.
Aliishawishi Mahakama Kuu ya Allahabad kumwachia Vijaya, na hatimaye
akapatiwa dhamana na kuungana tena na kijana wake nje ya kuta za gereza
hilo Mei 5.
"Habari ya Vijaya inashangaza. Mtoto wake wa kiume, alizaliwa jela,
mwishowe akamtoa humo," alisema mkuu wa gereza la Nari Niketan, Shashi
Srivastava.




