Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Thursday, May 30, 2013

MASKINI KUPA! SIKU CHACHE BAADA YA NDOA YAKE ALAZWA HOSPITALI KWA UGONJWA WA FIGO.SOMA STORI NZIMA HAPA

Na Imelda Mtema
MASKINI! Mwigizaji Idrissa Makupa ‘Kupa’ yuko katika wakati mgumu akiwa amelazwa katika Hospitali ya Tabata General, jijini Dar baada ya kugundulika ana tatizo kwenye figo.
Mwigizaji Idrissa Makupa ‘Kupa’.
Akizungumza na paparazi wetu kwa tabu, Kupa alisema alianza kujisikia vibaya akapima malaria na vitu vingine havikuonekana ndipo alipofanyiwa uchunguzi zaidi na kugundulika kuwa ana tatizo kwenye figo.
 
Kupa akiwa hospitali.
“Nilipopimwa zaidi nimegundulika kwenye figo kuna mawe madogomadogo, mpaka sasa wanafanya utaratibu wa matibabu ili Mungu akijalia nipone,” alisema Kupa ambapo mkewe, Mary anayemuuguza naye akionesha kuguswa na tatizo hilo.
“Yaani hapa nilipo hata chakula hakipiti, naomba Mungu amjalie mume wangu apone haraka,” alisema Mary.
Wawili hao walifunga ndoa siku chache zilizopita.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...