Kocha
 Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen leo (Mei 16 mwaka huu) ametaja kikosi 
cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kujiwinda kwa mechi ya mchujo ya 
Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini 
Marrakech, Morocco.
Katika
 kikosi hicho, Kim ameita wachezaji wapya sita ingawa baadhi yao 
wamewahi kuchezea timu hiyo, huku akiacha wengine watatu aliokuwa nao 
kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Morocco ambapo Taifa Stars ilishinda 
mabao 3-1.
Wapya
 aliowaita katika kikosi hicho kitakachoingia kambini Mei 20 mwaka huu, 
saa 1 jioni kwenye hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam ni Ally 
Mustafa, Vicent Barnabas, Juma Luzio, Haruna Chanongo, Mudhathiri Yahya 
na Zahoro Pazi. Wachezaji aliowaacha ni Shabani Nditi, Nassoro Masoud 
Cholo na Issa Rashid.
Kikosi
 kamili cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager 
ambacho kabla ya kwenda Morocco kitapita jijini Addis Ababa, Ethiopia 
kucheza mechi ya kirafiki Juni 2 mwaka huu dhidi ya Sudan ni kama 
ifuatavyo;
Makipa
 ni nahodha Juma Kaseja (Simba), Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa 
(Yanga) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Erasto 
Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Shomari 
Kapombe (Simba), Vicent Barnabas (Mtibwa Sugar) na Waziri Salum (Azam).
Viungo
 ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), 
Haruna Chanongo (Simba), Khamis Mcha (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), 
Mudathiri Yahya (Azam) na Salum Abubakar (Azam).
Washambuliaji
 ni John Bocco (Azam), Juma Luzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP 
Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), 
Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya 
Kidemokrasi ya Congo- DRC) na Zahoro Pazi (JKT Ruvu).
Kocha
 Kim amesema kikosi kitakachoingia kambini kitakuwa na wachezaji 24 
ambapo Samata na Ulimwengu watajiunga na timu jijini Marrakech, lakini 
wachezaji atakaondoka nao Dar es Salaam kwenda Addis Ababa ni 22 ambapo 
ataacha kipa mmoja na mchezaji mmoja wa ndani.
Awali
 TFF ilikuwa imeitafutia Taifa Stars mechi ya kirafiki Juni 1 mwaka huu 
dhidi ya Algeria, Libya au Misri. Lakini baadaye Algeria ikasema 
itacheza na Togo, wakati Misri ilitaka mechi hiyo ichezwe Juni 4 jijini 
Cairo, jambo ambalo lisingewezekana kwa Stars kwani ina mechi ya 
mashindano Juni 8 mwaka huu.
Kwa
 upande wa Libya mechi hiyo ilikubaliwa ichezwe Tunis, Tunisia, Juni 2 
mwaka huu. Lakini baadaye Libya ikataka mechi hiyo ichezewe jijini 
Tripoli ambapo TFF ilikataa kutokana na sababu za kiusalama.




