Mpaka muda huo kocha huyo aliyewahi kuinoa Chelsea na ambaye kwa sasa yupo Real Madrid hataweza kuongea hadharani kuhusu deal hiyo. Mourinho bado ana mkataba na Real lakini atarejea Stamford Bridge kwa kitita cha paundi milioni 10 kwa mwaka.
SunSport iliripoti kuwa mmiliki wa Blues tajiri Roman Abramovich alionekana hivi karibuni kwenye dinner na kocha huyo kwneye mgahawa wa La Famiglia, Chelsea. Mchezaji Wesley Sneijder, aliyenolewa na Mourinho Inter Milan, aliwahi kusema kuwa kocha huyo anaipenda sana Chelsea.



