Mlimbende Winlady White Mushi ndie aliyefanikiwa kunyakua taji la Redds miss Moshi 2013.
Hawa ndio warembo waliofanikiwa kuingia
tatu bora kwenye Redds Miss Moshi 2013 ambapo washindi hawa ndio
wataiwakilisha wilaya ya moshi katika kumsaka Miss Kilimanjaro 2013..
Hawa ndio walimbende walioingia tano
bora kwenye Redds miss Moshi 2013 na kupata nafasi za kuweza kuulizwa na
kujibu maswali ili kuweza kuwapata washindi watatu ambao wataiwakilisha
wilaya ya moshi.
Winlady White Mushi ambaye ndio Redds miss Moshi 2013/2014 akijibu swali.
Hawa ni baadhi ya warembo wa Redds
kutoka katika wilaya tofauti tofauti mkoani Kilimanjaro ambao wataungana
na warembo wa Redds Miss Moshi 2013 katika mtanange wa kumsaka Miss
Kilimanjaro 2013..
Winlady White Mushi "Redds miss Moshi
2013/2014" akionyesha kipaji chake na hapo alikua akicheza nyimbo yenye
mahadhi ya kihindi.
Huyu ndio aliyekuwa Redds Miss Moshi 20122/2013 akisubiri kumkabidhi taji Redds Miss Moshi 2013/2014.
Presenters wa Redds Miss Moshi 2013/2014 wakiwa na washiriki wa Redds Miss Moshi waliofanikiwa kuingia tatu bora.
Hawa walikua ni baadhi ya wanafunzi
kutoka chuo cha MUCCoBS wakishangilia kwa furaha baada ya Winlady White
Mushi kutangazwa kuwa ndio mshindi wa Redds miss Moshi 2013/2014 ambaye
mshiriki huyo ni mwanafunzi katika chuo cha MUCCoBS.
Msanii aliyepamba jukwaa alikua ni Dully Sykes aka Mr. Misifaaa....
Presenter mdogo lakini mwenye mambo
makubwa aliyeweza kuhakikisha kila jambo analolizungumza litakua na
umakini mkubwa na kuhakikisha kila aliyefika katika ukumbini wa Aventure
Africa anapata burudani na kuondoka akiwa na hamu kubwa ya kuendelea
kuburudika, alikua ni Kacim Mwinyi maarufu kama Babi D'e Conscious.