Imekuwa kama mazoea kwa Watanzania wengi
pindi wanapomuona Kijana mwenzao amefanikiwa huwa wanaanzisha story
tofauti. Hii imetokea kwa watu wengi sana hapa mjini na pengine kuchafua
kabisa majina yao maana maneno hayo yamekuwa yakitawala akilini mwa
watu siku hadi siku na kuwajengea imani kuwa ni kweli.
Robby ambae ni mfanyabiashara maarufu wa
maduka ya nguo Jijini Dar es salaam amekuwa ni mmoja wa watu ambao
wanasumbuliwa sana na tuhuma za kuwa ni member wa Freemason, katika
kupata ukweli wa jambo hili leo nimeongea na Robby One kuhusu issue
nzima ya watu kumuhisi yeye ni Freemason kutokana na maendeleo /
mafanikio yake makubwa katika biashara yake.
Robby amefunguka na kusema kuwa si kweli
kwamba yeye ana sali kwenye kanisa la Freemason wala hana uhusiano na
Jumuiya hiyo, pia anashangazwa na watu wanaomzushia maneno kuwa yeye ni
mwanachama. "Nashangaa vijana wananipigia simu mara nyingi na kuniomba
niwapeleke kwenye Kanisa la Freemason ninalo sali" alisema na kuongezea
"Naomba vijana wenzangu tuachane na hizi habari na kunipigia simu
kuniomba niwapeleke kweye hilo kanisa maana sijui lilipo wala sina
uhusiano nalo"
Moja kati ya ujumbe wa meseji aliotumiwa
ni huu " Naomba kuuliza samahani lakini felmasn wako wapi? naomba
nisaidie kama unawajua samahani lakini " ujumbe huo umetumwa kutoka
namba 0*** ****42
Amewataka vijana wa Kitanzania wafanye
kazi kwa bidii na kuachana na habari za uzushi ambazo zinawapotezea muda
wao, Siri kubwa ya mafanikio yake ni kufanya kazi kwa bidii na sio kama
wanavyodhani baadhi ya watu.