MWIGIZAJI
Mahiri wa filamu Bongo Wema Abraham Sepetu ndiye msanii anayelipwa
fedha nyingi kuliko msanii yoyote wa filamu katika kushiriki katika
filamu kutoka kwa watayarishaji wengine ili uweze kumshirikisha Wema
Sepetu katika filamu yako kama mwigizaji bila kujali anacheza scene
ngapi gharama yake ni milioni kumi.
Wema
ambaye kwa sasa anamiliki kampuni yake ya utengenezaji wa filamu
inayojuklikana kwa jina la Endless Fame Film anasema kuwa moja ya sababu
inayomfanya aweze kuchaji gharama hiyo inajumuisha na kutumia kampuni
yake pamoja yeye mwenyewe kuigiza katika filamu hiyo, kwa hiyo ni wajibu
wa mhusika kumudu gharama hizo.
“Yaah
kama mtayarishaji ananihitaji kushiriki katika filamu yake atatakiwa
kunilipa kiasi cha shilingi milioni kumi kwa kushiriki katika filamu
yake, lakini pia kuzingatia ratiba ya utendaji usiingiliane na kazi
zangu nyingine,”alisema Wema.
Inasemekana kuwa Wema ndio
msanii wa
kike anayeuza filamu kuliko mwigizaji wa filamu wa kike, pengine ndio
sababu ya kuweza kutoza gharama kubwa katika kushiriki filamu nje ya
kampuni yake unapomuhitaji Wema kwa ajili ya mapatano unaongea na
mtendaji wake wa karibu Chiddy Classic.
Gharama
hizo ndio kubwa kwani hadi sasa msanii ambaye amelipwa kwa kiwango cha
juu ilikuwa ni milioni tano ikiwa kama ndio kikomo cha malipo kwa
wasanii wenye majina na wamiliki wa makapuni yao, msanii kama Ray the
Greatest hanunuliki kwani si rahisi kushiriki nje ya kampuni yake ya RJ
Company.