Kabla ya kuingia magofu hayo ya kale unakutana na tangazo hili
Sehemu ya Choo
Mzee Mohamed Pazi [80] ambaye amezaliwa na kukulia kijiji hicho cha Kaole,akiwa nje ya ofisi za makumbusho hayo
Baada ya muda Mtandao huu ulimshuhudia Mzee Mohamed Pazzi akiingia kwenye Msikiti huo wa kale.
Akiingia ndani
Sehemu ya Kibla ya msikiti huo wa kale uliojengwa kalne ya 13
Mzee Pazzi akiswari kwenye msikiti huo wa Kale eneo la Kibla
Pia Mtandao huu
uliwashuhudia baadhi ya watalii wa ndani wakinawa maji ya baraka
yaliopo eneo la Msikiti huo kwa lengo la kujisafisha na kweda kuswari
kwenye msikiti huo wa kale
Watalii hao wa ndani wakiswari kwenye Msikitim huo
Sehemu ya msikiti huo
ambayo pembeni yake kuna kisima chenye maji ya baraka,
Sehemu ya Msikiti huo uliojengwa karne ya 13 ikumbukwe hii ni karne ya 21
Akizungumza na Mtandao huu kwenye mahojiano maarumu Mzee Mohamed Pazzi[80] Mkazi wa kijiji hicho,alidai kwamba toka azaliwe miaka 80 iliyopita kwenye kijiji hicho hajashuhudia maji hayo yakipungua au kuongezeka.
" Mimi nimezaliwa hapa miaka 80 iliyopita sijashuhudia maji haya wakipungua au kuongezeka toka karne hiyo ya 13,ambapo toka kipindi hicho mvua nyingi zimenyesha lakini hajaongezeka pia jua kali la toka kipindi hicho cha kalne ya 13 mpaka sasa alijaweza kukausha hata tone la maji hayo huku makundi ya watu wakichota maji hayo kila siku lakini pia hayajapungua"alisema Mzee huyo
Vile vile mzee huyo alieleza maajabu mengine yaliopo kwenye msakiti huo alidai kwamba kwa maelezo ya mababu zake Msikiti huo ulikuwa wa maajabu ambapo Sheikh aliyekuwa akiazini alipanda juu ya ngazi hizo na kuazini bila kipaza sauti lakini sauti yake ilifika umbali mrefu.
" Mababu na mabibi zetu walitueleza kwamba Muazini alikuwa akipanda juu ya ngazi hizi alipoazini swara ile ya alfajiri sauti yake ilifika mbali sana kutoka eneo hili hadi Chalinze wakati mwingine sauti ilifika mikoa ya jirani kama Morogoro na Dar es salaam, wazee hao waliongeza kusema kwamba Sheikh aliazini bila kipaza sauti lakini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu subuhana wa taara sauti hiyo ili peperushwa na upepo na kufika maeneo hayo ya mbali"aliongeza kusema Mzee Pazzi.



