| Dk. Willibroad Slaa na mchumba wake, Josephine Mshumbushi. |
Na Happiness Katabazi, Dar es salaam
HATIMAYE
Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, imetupilia mbali rufaa iliyokuwa
imekatwa na aliyekuwa mume wa Josephine Mushumbusi, Maimbo baada ya
kuiona rufaa hiyo haina msingi wowote kisheria.
Hukumu
hiyo ya rufaa ya madai ya ndoa Na.32/2012 ilitolewa leo na Hakimu
Aniseth Wambura ambapo alisema mahakama yake imefikia uamuzi huo wa
kuitupa rufaa hiyo kwasababu haina mantiki ya kisheria.
Hakimu
Wambura alisema mahakama yake imekubalina na hukumu iliyotolewa Aprili
2012 na Mahakama ya Mwanzo Sinza katika kesi ya madai talaka iliyokuwa
imefunguliwa na Mushumbusi anayetetewa na wakili wa kujitegemea Philemon
Mutakyamilwa dhidi ya Maimbo ambapo mahakama hiyo ya chini ilitangaza
kuwa hakukuwa na ndoa baina ya watu hao kwasababu Maimbo alikuwa ni
mzinzi, simwaminifu katika ndoa yake na alikuwa akimtesa mkewe.
“Baada
ya mahakama yangu kusikiliza hoja za mwomba rufaa na mjibu rufaa
,mahakama hii imefikia uamuzi wa kukubali hoja za Mushumbisi kuwa kwa
tabia ile ya mbaya ya uzinzi na ukosefu wa uaminifu katika ndoa yake
hapakuwepo na ndoa baina yao hivyo mahakama yake inatangaza kuwa hukumu
ya mahakama ya Mwanzo Sinza ambayo iliivunja ndoa hiyo ilikuwa hukumu
sahihi “alisema hakimu Wambura.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo wakili
Mutakyamilwa alisema amefurahishwa na hukumu hiyo kwani mahakama
imetenda haki kwasababu kesi hiyo ya madai ya talaka ilikuwa na msukumo
wa siasa chafu zilizokuwa na lengo chafu la kumchafulia jina mteja
wake(Mshumbusi) ambaye kwa sasa ni mzazi mwenzie Katibu Mkuu wa Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.Wilbroad Slaa.



