Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Zaipora Pangani akiongea kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya wiki ya fistula leo mjini Bukoba. Wa kwanza kulia ni Balozi wa Chapa Vodacom Msanii Mwana FA na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacam Salum Mwalim. Wengine pichani kushoto ni Mwakilishi wa CCBRT Kasper Mmuya na Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Nassor Mnambila.Maadhimisho hayo yanafadhiliwa na Vodacom, Vodafone na CCBRT
Wakazi wa
Mji wa Bukoba waliofurika kushuhudia uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya
wiki ya fistula uliofanywa leo mjini humo kueleka siku ya fistula
duniani Mei 23. Maadhimisho hayo yanaratibiwa na kufadhiliwa na
Vvodacom, Vodafone na CCBRT yakiwa na ujumbe "Fistula inatibika,
jitokeza upate matibabu bila ya malipo
Mkuu wa
Wilaya ya Bukoba Zaipora Pangani akikabidhi funguo ya gari kwa Balozi wa
Chapa Vodacom Msanii Mwana FA tayari kuanza safari ya kuanza Bukoba
kwenda Dar salaam kupitia mikoa mbalimbali kuelimisha jamii juu ya
tatizo la fistula na jinsi matibabu yanavyopatikana bila malipo katika
hospitali ya CCBRT kwa ufadhili wa Vodacom. Kulia ni Katibu Tawala wa
Mkoa wa Kagera Nassor Mnambila na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom
Salum Mwalim.Kilelele cha maadhimisho hayo kitafanyika Mei 23 siku ya
fistula duniani.