Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe |
Kutokana na hali hiyo, hotuba iliyokuwa isomwe na
Serukamba kama maoni ya kamati baada ya Dk Mwakyembe kuwasilisha hotuba
yake, ilibadilishwa dakika za mwisho na kusainiwa na Makamu Mwenyekiti
wa......... Kamati hiyo, Profesa Juma Kapuya.
Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo (ambaye aliomba
jina lake lihifadhiwe) alisema waliamua kuunda kamati ndogo ya wabunge
wanne kusahihisha lugha iliyotumika katika kuandaa maoni ya kamati hiyo
kuhusu Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka wa Fedha wa
2013/2014.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, wajumbe waligundua
kuwa lugha iliyotumika ililenga kushambulia moja kwa moja Dk Mwakyembe
ndani ya Bunge jambo ambalo lilkuwa kinyume cha makubaliano ya kamati.
Hata hivyo, Serukamba akizungumza na gazeti hili
alikana kubadili hotuba hiyo na kuongeza kuwa; “Mimi nimerudi jana, kwa
kawaida kamati ikishajadili suala la hotuba kuandikwa tunamwachia Katibu
na akimaliza anairudisha kwetu wabunge. Hivyo nilichokisoma ndicho
tulichokubalina na wajumbe wa kamati hiyo.”
Aliongeza: “Msitake kunigombanisha na mheshimiwa
Waziri, mimi ndiyo kwanza nimeingia asubuhi hii hakuna kilichobadilika
katika hotuba hiyo.”
Gazeti hili lilifanikiwa kuona nakala mbili za
hotuba za kamati, moja ikiwa na saini ya Serukamba na nyingine ikiwa
imesainiwa na Profesa Kapuya na zote zina tarehe inayofanana ambayo ni
Mei 16, 2013.
Kwa upande wake Kapuya katika majibu ya maandishi
kwa gazeti hili alisema si kweli kwamba ziliandikwa hotuba mbili.
“Habari hizo hazina ukweli, kamati yangu ina utaratibu wa kuandaa hotuba
yetu na ikishakamilika tunateua kamati ndogo ambayo inapitia hotuba
hiyo kabla ya kuisoma,”alisisitiza Profesa Kapuya.
Majibu ya Serukamba na Kapuya yanatofautiana na
kauli ya Dk Mwakyembe ambaye aliliambia gazeti hili kwamba pia alipata
taarifa za kuwapo kwa mpango huo kutoka kwa “watu wanaojua na kuthamini
kazi yake.”
“Siyo kila mtu anaweza kukuchukia huwezi kunyimwa
maneno, watu wenye imani na mimi walikuja kunipa taarifa na wakanipatia
ile aliyokuwa ameandika yeye…. ana bahati sana nilikuwa namsubiri kwa
hamu aisome hiyo hotuba yake nilipanga kumchanachana pale pale
asingeamini,”alisisitiza Dk Mwakyembe.
Alipoulizwa kwa nini anafikiri mwenyekiti huyo
ameamua kumfanyia hivyo, Dk Mwakyembe alisema; “Siwezi kujua lakini
naamini hizi ni mbio tu za mwaka 2015.”
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema hafahamu
kuhusu suala hilo. “Ninachofahamu ni kwamba Serukamba alikuwa amesafiri
kwenda China na mimi nilimwona siku hiyo akisoma maoni ya kamati yake,
kama kulikuwa na tatizo hilo pengine litakuja baadaye ofisini
kwetu,”alisema Ndugai kwa simu.
Ilikuwaje?
Habari zinasema licha ya kwamba Serukamba alikuwa nje ya nchi, alihusika katika kuandaa rasimu ya awali ya taarifa ya kamati ambayo yeye alisaini.
Habari zinasema licha ya kwamba Serukamba alikuwa nje ya nchi, alihusika katika kuandaa rasimu ya awali ya taarifa ya kamati ambayo yeye alisaini.
Hata hivyo wakati akiwa bado hajarejea nchini,
wajumbe wa kamati yake walibaini kwamba katika hotuba hiyo kulikuwa na
lugha ya kumuhoji zaidi waziri pamoja na Serikali badala ya kushauri,
huku baadhi ya kauli zikionyesha kumlenga Dk Mwakyembe binafsi.
Wajumbe hao walilalamika kwamba maneno hayo
yaliyokuwa yakimshambulia waziri ni kinyume na walivyokubaliana hivyo
waliamua kuunda kamati ya watu watatu ambao ni wajumbe wa kamati hiyo
ili kufanya marekebisho.
“Hatua ya kuunda kamati hiyo ndogo ilifikiwa
Jumatatu wiki hii, maana tulibaini kwamba lugha iliyotumiwa haikuwa
sahihi, sisi kazi yetu ni kuishauri Serikali na si kuhoji maswali,
maswali unaweza kuhoji wakati wa kuchangia mbunge mwenyewe lakini si kwa
kuandika katika maoni ya kamati, “kilieleza chanzo hicho.
Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge toleo la 2007 ya
114(18), Kamati ya Kudumu ya Bunge inaweza kuunda kamati ndogo kwa ajili
ya utekelezaji bora wa shughuli zake, kadri itakavyoona inafaa na kila
kamati ndogo itapangiwa kazi zake na kamati ya kudumu husika.
Wajumbe hao ni Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ramo
Makani na Wabunge wa Viti Maalumu, Rita Kabati na Zarina Madabida wote
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Hotuba hiyo baada ya kukamilika ilisainiwa
na Profesa Kapuya na hiyo ndiyo iliyosomwa bungeni.