MSANII wa muziki wa Bongo fleva, Abubakari Katwila, ‘Q Chillah’(Pichani) leo anatarajiwa kuwasha moto wa burudani katika klabu ya kimataifa ya burudani ya Bilicanas sambamba na kufanya ‘shooting’ ya video ya wimbo wake ‘Beautiful’.
Chillah amesema kuwa amejipanga vema na atasindikizwa na baba yake mzazi, Shabani Katwila, ambaye hivi karibuni ametangaza kumaliza bifu walilokuwa nalo.
Wasanii wengine ni Makamua na Bee Man kutoka nchini Kenya.
Chillah aliwataka mashabiki wajitokeze kwa wingi leo Bills na kwa watakaotaka kuonekana katika video ya ‘Beautiful’ watapewa uwanja.
“Watu watarajie kumuona Chillah katika ngazi za kimataifa, si yule wa zamani, sasa ni mpya, watapata shoo kali nikiwa sambamba na wachezaji wangu, na pia video tutaanza kui-shoot nje na baadaye katika stage,” alisema Chillah.
Katika onesho lake lililopita, Chillah pia alimpandisha baba yake mzazi, Bw Shaaban Katwilla jukwaani na kuleta msisimko mkubwa katika oneshon lake hilo lililofanyika Maisha Club