Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Thursday, May 30, 2013

BIBI KIZEE WA MIAKA 65 AFARIKI DUNIA AGONGWA NA GARI,NI MMOJA KATI YA WALE WALIODHANIWA WACHAWI WALIOANGUKA MHONGOLO WILAYANI KAHAMA

BIBI MWAJUMA MPONI AKIWA HOI MARA BAADA YA KUGONGWA NA GARI LA MAJI

 


WAZEE WANAOSADIIWA KUWA NI WACHAWI WAKIWA CHINI YA ULINZI KITUO CHA POLISI,KUTOKA KUSHOTO NI SHIJA NKWABI (80) NA MWAJUMA MPONI (65).

Bibi huyo baada ya kuachiwa toka kituo cha Polisi alikuwa analala katika vibaraza vya maduka mjini kahama wakati wa usiku na mchana hupendelea kulala chini ya miti au chini ya magari yaliyopaki.
Kwa mujibu wa madreva wanaopaki magari yao eneo hilo wameiambia blog hii kuwa hata wao walishawahi kumkosa kumgonga mara nyingi katika eneo hilo.

MATUKIO KATIKA PICHA

ASKARI WA USALAMA BARABARANI WAKICHUKUA MAELEZO TOKA KWA MASHUHUDA.

BIBI MWAJUMA AKIWA HOI BAADA YA KUKANYANGWA NA GARI

POLISI WAKIWA KATIKA HARAKATI ZA KUMPELEKA HOSPITALI BIBI HUYO

AISEEE INASIKITISHA SANA

MGUU WA KULIA WA BIBI HUYO UKIWA UMEKATIKA KABISA NA KUSHIKILIWA NA NGOZI TU


VIJANA WA KAHAMA MJINI WAKIWASADIA POLISI KUUPAKIA MWILI HUO KWENYE GARI.

BIBI MWAJUMA AKITEREMSHWA HOSPITALINI.
HAPA VIJANA WA KAHAMA WAKIMSUKUMA BIBI HUYO KUMUINGIZA HOSPITALINI ,TAFADHALI USINIULIZE MANESI NA MADAKTARI WALIKUWA WAPI KUTEKELEZA JUKUMU LAO.
VIJANA WAKIENDELEA KUJITOLEA KUMSAIDIA BIBI HUYO ILI AWAHI KUPATA MATIBABU,SWALI LANGU NI JE WANA UZOEFU WA KUSUKUMA WAGONJWA KATIKA MAGARI HAYO?
 
KAHAMA
Bibi mmoja aliyefahamika kwa jina la Mwajuma Mponi anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 75 hadi 80 amefariki dunia leo baada ya kukanyagwa na gari la maji taka wilayani Kahama, mkoani Shinyanga.
Kwa mujibu wa mkuu wa polisi wilayani Kahama, Gerge Simba, Bibi huyo amekanyagwa leo mchana maeneo ya nyuma ya hospitali ya wilaya hiyo wakati akiwa amelala chini ya gari hilo kwa ajili ya kivuli.
Simba amesema Bi Mwajuma amefariki dunia mida ya saa moja jioni leo wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Kahama kutokana majeraha makubwa yaliyompata ikiwemo kuvunjika vibaya mguu wake wa kulia.
Hata hivyo Simba ametoa wito kwa madereva kuwa makini na kuhakikisha wanakagua chini magari yao sehemu wanapopaki au kupiga honi kabla ya kuondoka kwani ni hatari kwa wazee wanaokuwa wanajizuia jua na hata kwa watu wengine.
Amesema dereva wa gari hilo ambaye alikimbia kufuatia tukio hilo, kwa sasa anashikiliwa na polisi kwa mahojiano baada ya kukamatwa jioni hii maeneo ya Kahama mjini.
Kumbukumbu zimebaini kuwa Bibi huyo ni mmoja kati ya wale walioanguka April 3 katika kata ya Mhongolo wilayani Kahama na kupelekwa polisi kwa kudhaniwa kuwa ni wachawi.
Bibi huyo baada ya kuachiwa toka kituo cha Polisi alikuwa analala katika vibaraza vya maduka mjini kahama wakati wa usiku na mchana hupendelea kulala chini ya miti au chini ya magari yaliyopaki.
 
Credits: Kb blog
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...