Franck
Ribery ameapa kutoongea tena na mchezaji mwenzie wa Bayern Munich Jerome
Boateng baada ya kulowanishwa kwa pombe wakati wa wakishangilia ubingwa
wa Bundesliga wikiendi iliyopita.
Mfaransa
huyo ambaye ni muislamu wa swala tano - alijaribu kukimbia ili aepuke
ushangiliaji wa kumwagiana pombe wa wachezaji wenzie baada ya filimbi ya
mwisho ya mchezo walioshinda 3-0 dhidi ya Augsburg.
Lakini
pamoja na kujaribu sana kukwepa kuguswa na pombe - ambayo ni haramu kwa
dini yake - Ribery hatimaye aliogeshwa na na Boateng.
Akiwa
amekasirishwa kabisa kwa kitendo hicho cha mjerumani, winga huyo
alisema: ‘Sitoongea tena na Boateng, anajua mie muislam. Nimeudhiwa sana
na kitendo chake.’
Mlinzi
David Alaba na kiungo Anatoliy Tymoshchuk pia walijiunga na Boateng
kumlowesha Ribery, ambaye alionekana kutulia kwa wakati huo.
Golikipa
Manuel Neuer kwa busara kabisa yeye alijiepusha na suala hilo na kuamua
kuwamwagia baadhi ya mashabiki walionekana kupendezewa na ushangiliaji
huyo.