Akiongea
na waandishi wa habari Ofisi kwake hii leo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Lindi,George Mwakajinga alieleza kuwa Watuhumiwa hao waliojitambulisha
kwa Rajabu Juma Mbete(26) mkazi wa manispaa ya Lindi na Hamis
Athuman(32) mkazi wa Mbembetini Kibiti Mkoani Pwani licha ya kupora simu
6 na fedha taslim laki 6 pia walimjeruhi kwa Mapanga Bw Hamis Hassan
Muuza duka hilo.
Mwakajinga
alibainisha kuwa Majambazi hayo yanayosadikiwa kuwa 4 walifanikiwa
kukimbia baada ya Bunduki waliyokuwa nayo kugoma kufyetua risasi hali
iliyofanya wanavijiji vya Kitomanga,Mkwajuni na Mbwemkuru kuanza msako
na kufanikiwa kuwakamata na kuwajeruhi kwa kuwapiga na kuwachoma moto
kabla hawajapata msaada wa Jeshi la Polisi.
Akielezea
kuhusu kukutwa na risasi tatu za Shortgun,Bangi pamoja na Bunduki aina
ya Shortgun ya kienyeji, Kamanda mwakajinga alifafanua Bunduki hiyo
Ambayo hutumia risasi za Short gun pia walikutwa na risasi 3.
Watuhumiwa
hao ambao wamelazwa huku wakiwa chini ya Ulinzi wa Jeshi la Polisi
watafikishwa mhakamani mara baada ya Afya yao Kuimarika kutokana
kunusurika kuchomwa Moto na Wananchi ambapo tayari wameweza kutambuliwa
na baadhi ya wanakijiji



