Na ELIPHACE MARWA na FRANK SHIJA – MAELEZO
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala Muungano Mh.
Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa watanzania kujitokeza kwa wingi
kesho katika maadhimisho ya miaka 49 ya muungano wa Tanganyika na
Zanzibar.
Ametoa
kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na waandishi
wahabari kuzungumzia maadhimisho hayo yatakayofanyika kesho katika
uwanjwa wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Amesema
kuwa kesho ni siku muhimu kwa Watanzania kuenzi na kuudumisha Muungano
kwa kuwa umesababisha Tanzania kupata heshima kubwa Afrika na duniani
kote.
“Ninatoa
wito kwa wananchi wote kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya miaka
49 ya Muungano wetu, kwani hakuna asiyejua kuwa Muungano huu umetuletea
heshima kubwa kimataifa, hivyo ni wajibu wetu kuulinda na kuudumisha”
amesema Mh. Samia.
Aidha
Waziri huyo amesema kuwa pamoja na changamoto zilizopo Muungano
umeendelea kuimarika kwa kuwa wananchi wana imani kubwa na Muungano huu
na Serikali imeendelea kushughulikia kero mbalimbali za Muungano.
Mh.
Samia ameongeza kuwa katika kushughukia kero zilizopo katika Muungano ,
Serikali ya awamu ya tatu mwaka 2004 iliunda kamati yenye wajumbe
kutoka pande mbili za Muungano ya kushughulikia kero hizo.
Aidha,mwaka
2006 kamati hiyo ilianza kushughulikia kero hizo mpaka sasa jumla ya
hoja tisa kati ya hoja 13 za Muungano zimekwisha kamilika na kupatiwa
ufumbuzi.
Muungano
wa Tanganyika na Zanzibar uliasisiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume tangu tarehe
26/04/1964 ambapo kesho unatimiza miaka 49