Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Marceline Magesa
(kulia) akizungumza katika hafla ya uwekaji saini mkataba wa ujenzi wa
kivuko cha Dar es Salaam- Bagamoyo leo jijini . Kivuko hicho kitakuwa
na uwezo wa kubeba watu 300 , kitagharimu shilingi7.91
bilioni.(bilioni7.91 za tz).Pichani kutoka kulia ni Waziri wa Uchukuzi
Dkt,John Magufuli,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mecky Sadick, na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi , Balozi Herbert Mrango.
Mtendaji
Mkuu wa TEMESA Mhandisi Marceline Magesa (mwanamke) , na mwakilishi wa
kampuni ya JOHS GRAM HANSSEN A/S ya Denmark Andreas Gottrup wakiweka
saini mkataba wa ujenzi wa Kivuko cha Dar es Salaam- Bagamoyo leo
jijini Dar es Salaam, katika hafla iliyoshuhudiwa na Waziri wa Ujenzi
Dkt. John Magufuli (aliesimama katikati) Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Mecky Sadick(alie vaa shati la kitenge) Balozi wa Denmark nchini
Tanzania Mh, Johnny Flinto (mzungu aliesimama mstari wa nyuma). Pamoja
na watendaji wakuu wa Wizara ya Ujenzi.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Sadick Mecky (kulia) akizungumza wakati wa
hafla ya uwekaji saini mkataba wa ujenzi wa Kivuko cha Dar es salaam –
Bagamoyo. Kivuko hicho kitagharimu shilingi 7.91 bilioni za kitanzania.
Mwengine ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (kulia) akiongea na Balozi wa Denmark
nchini Tanzania Mh. Johnny Flinto,katika sherehe ya uwekaji saini
mkataba wa ujenzi wa kivuko cha Dar es Salaa- Bagamoyo (April 25, 2013).
Mwenyekiti
wa Bodi ya ushauri ya TEMESA, Prof. Idrisa Mshoro (kulia) akimueleza
jambo Mwakilishi wa kampuni ya JOHS GRAM HANSSEN A/S ya Danmark ,
Andreas Gottrup wakati wa sherehe za uwekaji saini mkataba wa ujenzi wa
kivuko cha Dar es Salaam- Bagamoyo jijini Dar es Salaam(April,25,2013).
waziri wa ujenzi Dr. John magufuli akiongea ktk hafla