Katika
habari hiyo, mtu aliyetajwa kwa jina la Everson Makowa (49) ambaye ni
meneja wa kampuni ya kusafirisha mizigo ya Malawi Cargo tawi la mkoani
hapa alidaiwa kunaswa gesti na mke wa mfanyakazi wake .
Sasa, habari mpya ni kwamba bosi
huyo ambaye pia ni mbunge mstaafu wa Jimbo la Nkotakota South East
nchini mwake anadaiwa kupigwa chini kazini kwake baada ya uongozi wa
kampuni hiyo makao makuu yaliyopo nchini Malawi kuzinyaka taarifa za
kudaiwa kufumaniwa na mwanamke huyo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu,
mara baada ya habari hiyo kutoka mtandaoni, uongozi wa kampuni hiyo
ulimwandikia barua ya kumwachisha kazi mtuhumiwa huyo.
Mwandishi wetu Jumatano
iliyopita alikwenda nyumbani kwa mdaiwa huyo ambapo pia ndiko zilipo
ofisi za kampuni hiyo kwa lengo la kuzungumza naye lakini watu
waliokuwepo walisema alikuwa ametoka.
Kwa mujibu wa mfanyakazi mmoja
alikiri jamaa huyo kutemeshwa mzigo na kuongeza kuwa, tayari bosi
mwingine amefika kuziba nafasi yake.
Mwandishi wetu alipoomba azungumze na bosi mpya, aliambiwa alikuwa na wageni hivyo ikawa vigumu kumpata.
Pamoja na habari ya kutemeshwa
kazi, mtuhumiwa huyo ameshindwa kuondoka Mbeya kurudi Malawi kufuatia
kesi inayomkabili kutarajiwa kuunguruma mahakamani ambapo mume wa
mwanamke huyo ndiye mlalamikaji.
Siku ya tukio, majira ya saa
11:25 jioni, mtuhumiwa huyo alifika kwenye gesti hiyo akiwa ndani ya
gari aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajili T 821 ASY.
Mtego wa kumnasa jamaa huyo
uliandaliwa na polisi kwa kushirikiana na mume wa mwanamke, jamaa na
marafiki huku mke wa mlalamikaji akitoa ushirikiano wa kutosha.
Mwanamke aliyenaswa naye, mumewe alikuwa mfanyakazi wake wa ndani lakini alimsimamisha kazi kwa madai ya kuchelewa kazini.
Habari zinadai, tangu alipomsimamisha alikuwa akiomba penzi kwa mkewe akidai ndiyo ujira wa msamaha kwa mumewe.