Ubalozi wa Uingereza nchini Somalia wafunguliwa tena
Ubalozi wa Uingereza nchini
Somalia umefunguliwa tena. Huu ni ubalozi wa kwanza wa nchi za Umoja wa
Ulaya kufunguliwa nchini Somalia.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Bw. William Hague amesema,
huu ni mwaka wa 22 tangu wanadiplomasia wa Uingereza kuondoka nchini
Somalia, na kufunguliwa tena kwa ubalozi huo kutafungua ukurasa mpya wa
uhusiano kati ya nchi hizo mbili.