Mkurugenzi
wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof John Nkoma akitoa hotuba
katika mkutano wa kujadili juu ya usajili wa namba za simu za mkononi .
Prof.
Nkoma katika mkutano huo alisema kwa kushirikiana na makampuni ya simu
watumiaji wote wa simu za mkononi ambao hawajasajili namba zao wafanye
hivyo mara moja, kwani utaratibu unaofuata ni kufunga namba zote ambazo
hazijasajiliwa.
Akifafanua
zaidi juu ya msimamo huo Nkoma alisema ni kosa la jinai kutumia namba
ya simu isiyosajiliwa na adhabu yake ni faini ya shilingi laki tano au
kifungo cha miezi mitatu jela.
Aidha amewataka wananchi kuhakiki usajili wao kwa kupiga nyota 106 alama ya reli, ili kujua kama wamesajiliwa.
mkutano huo ulifanyika makao makuu ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA) jijini Dar es salaam.