Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Friday, April 19, 2013

ANGALIA PICHA ZA MGAMBO ALIYEPEWA KAZI YA KULINDA KABURI KUTOKANA NA WIZI MAKABURINI

Mmoja wa wanafamilia akimpa maelekezo mlinzi huyo wa kaburi hilo la kifahari..
Kutokana na kukidhiri kwa vitendo vya wizi kwenye makaburi,familia ya marehemu mdaku imeamu kuweka mlinzi kulinda kaburi la mpendwa wao nyakati za usiku kwa lengo la kulinda vitu mbali mbali vya dhamani zilivyomo kwenye kaburi la mpendwa baba yao. Akihojiwa na audifacejackson blog wa habari hizi mgambo huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mganga Chigillo aliuthibitishia  kupewa kazi ya kulinda kaburi hilo vyakati za usiku kwa lengo la kupambana na vikaba wenye tabia ya kuvamiamakaburini vyakati za usiku na kuimba vitu mbali mbali.

 Mgambo huyo akitoa maelezo kwa familia ya mzee Mdaku,kulia ni mke wa marehemu na kushoto ni mtoto wa kwanza wa marehemu akiwa na mumewe..
Mgambo akielezea zaidi alimwambia audifacejackson blog Nikweli nalinda kaburi la mzee mdaku na kwamba kazi hiyo sio nyepesi mfano jana majira ya saa nanne usiku nimeshuhudiakundi la watu wake kwa waume wakiwa wamevamia nguo nyeupe wakizunguka kwenye makaburi .lakini kwa ujasiri sikukimbia badala yake niliendele kugonga pombe yangu aina ya  konyagi  niliweka dhana zangu jirani kama wangenilitea noma ningepambana nao kwa bahati nzuri walipomaliza shughuri zao waliondoka zao bila kusogea kwenye kaburi hili" alisema Mgambo huyo mwenye mke na watoto kadhaa.

                       Padri akizungumza na Mgambo huyo nje ya kaburi hilo


 Maneno haya ya busara yaliwekwa nyumba ya msaraba uliopo kwenye kaburi la mpendwa wetu Mzee Mdaku


 Baada ya kuhojiwa na mwandishi wa habari hizo Afande huyo alitoa rundo la viroba mfukoni na kudai kwamba kitu hicho ndichon pekee kinachompa ujasili wa kukaa makaburini usikukucha


 Baada ya kugonga viroba mfurulizo afande huyo alijikuta akiuchapa usingine wakati shughuri zikiendele kama alivyonaswa na kamera za Mtandao huu.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...