Simu za mkononi hutumika kwa mambo mengi ikiwemo kuongea na
watu wengine waliokupigia au uliowapigia, kutuma na kupokea ujumbe mfupi wa
maneno, kutuma na kuokea picha au video, kuhifadhi kumbukumbu nakadhalika.
Licha ya simu za mkononi kuwa na matumizi mengi, swala la
kujua ni jinsi gani utaitumia ili
matumizi yako yawe ni yenye tija ni muhimu sana. Mfano kama utatumia simu
yako ya mkononi vizuri itakusaidia kurahisisha
mambo
mengi ambayo hayakulazimu wewe kuwa mahali husika na kutumia mikono
yako, kukuepusha wewe kusafiri sehemu moja kwenda pengine pasipo na
ulazima na mengine mengi yote ni katika kurahisisha kazi na kuokoa muda.
Haya ni mambo machache ya kuzingatia unapokuwa mtumiaji wa simu ya mkononi..
1. Kama huna ulazima wa kutumia simu wakati wote, panga muda
maalum wa kutumia simu yako.
-Kwa siku tunafanya kazi nyingi ikiwa simu ni moja wapo ya kifaa cha mawasiliano tunachotumia mara kwa
mara. Lakini wengi wetu tuna mazoea mabaya ya kutotumia simu vizuri,
kama huna ulazima wa kushika simu na kuitumia ni bora ukaendelea kufanya
kazi nyingine kuliko kupoteza muda wako muhimu kuchat au kufanya mambo
mengine kwenye simu ambayo hayakuwa kwenye ratiba yako ya kazi.
2. Unapokuwa na simu ya mkononi usipuuze kila mtu
anayekupigia.
-Wakati mwingine simu zinazopigwa ni muhimu kwako kupokea kwasababu huna
uhakika asilimia mia moja wa kile mpigaji simu anachotaka kukuambia.
Kama upo busy sana wataarifu watu wako muda wa kukupigia kwa kuwaeleza
muda ambao wanaweza kuwasiliana na wewe.
3. Kama simu yako inakuwezesha kupata internet, epuka
kuperuzi sana kwenye mtandao.
-Ni muda mwingi sana tunatumia kuperuzi tovuti mbalimbali za habari,
kazi na mitandao mingine ya kijamii ( facebook, twitter ). Mimi binafsi
ni muathirika wa kutumia internet kwa muda mrefu kwa siku. Ni vizuri
kama ukipanga muda maalum wa kuwa unatumia internet. Mfano: Tumia
muda wako kuangalia barua pepe kwenye mtandao angalau mara mbili(2) au
tatu(3) kwa siku kama kazi yako haikulazimu kutumia mtandao wa internet
muda wote.
4. Unapokuwa unaendesha chombo cha moto ( gari, pikipiki )
epuka kutumia simu.
-Ajali nyingi sana hutokea barabarani kwasababu ya uzembe wa kutokuwa
makini ukiwa barabarani. Unapokuwa barabarani ukiendesha gari, piki,
baiskeli epuka kutumia simu. Kama mtu anakupigia au umepokea ujumbe
mfupi wa maneno (message) na ni muhimu kwako kupokea ni vyema
ukasimamisha chombo unachoendesha na kufanya unachotaka kisha ukimaliza
ndio uendelee na safari.
5. Unapokuwa unaandika ujumbe mfupi wa maneno kwa mtu,
chunga usitumie lugha chafu.
-Kila mtu anamtazamo wake wa mambo, kuna kitu ambacho wewe unaona ni
sawa lakini kwa mweingine utakuwa umemkosea kabisa. Unapotaka kumtumia
mtu ujumbe (message) ni vyema ukaihakiki kabla ya kutuma, kufanya hivyo
utaepusha kutoelewana baina yako na mpokeaji wa ujumbe uliotuma.
6. Wakati wa maongezi kwenye simu, chunga usipayuke bali
ongea kwa sauti ya kawaida.
-Kama nilivyozungumzia kwenye mada iliyopita kuhusu kuongeza ujuzi wako
wa kuongea, kupayuka kunaweza kusababisha msikilizaji kukuchukilia
vibaya kuwa wewe ni mkali, una hasira au mgomvi. Badilisha sauti yako ya
maongezi iwapo tu unasisitiza kitu au unaonyesha hali fulani kuhusu jambo linazungumziwa.
7. Kama wewe unapenda sana kucheza michezo game(s) kwenye simu, epuka kutumia muda mwingi.
-Simu zetu za mikononi nyingi zina michezo mbalimbali ya kutuburudisha, usijizoeshe
kucheza game(s) kwa maana ya michezo kupita kiasi. Ukipata muda wa
kupumzika cheza game(s) kuchangamsha akili lakini usipitilize kucheza
kupita kiasi.
8. Kama itawezekana, jiwekee muda wako binafsi wa kuwa mbali
na simu. Si jambo zuri kila wakati uwe na simu labda kuwe na ulazima wa wewe kuwa karibu na simu muda wote.
-Kuna wakati unahitajika kukaa na watu wako wa karibu kama familia,
marafiki au jamaa zako, haipendezi kama utakuwa ukitumia simu ikiwa
wenzako wanatagemea uwe nao kwa wakati huo