Mama Anna Mkapa akiangalia moja
ya banda la kufugia kuku cha kikundi cha Engiterata Sidai kilichopo
kijiji cha Olgilai wilayani Arumery mkoni Arusha.
Mwenyekiti wa mfuko wa fursa
sawa kwa wote(EOTF),Mama Anna Mkapa akiangalia bidhaa za wajasiriamali
wakati alipotembelea kikundi cha akina mama cha Engiterata Sidai
kilichopo kijiji cha Olgilai wilayani Arumeru mkoani Arusha mwishoni mwa
wiki aliyevalia vazi la kimaasai ni mwenyekiti wa kikundi hicho,Janeth
Mollel
Picha ya pamoja na mgeni rasmi mama Mkapa
Mama Mkapa akiwa na wanakikundi katika eneo la ujasiriamali
Kamanda Moses Mashalla akinywa oloshoro
Hapa Mama Mkapa akiagana na wanakikundi mara baada ya kumaliza kutembelea kazi zao
Wajasiriamali nchini
wametakiwa kuzalisha bidhaa zenye ubora ili waweze kupata masoko ya
uhakika sanjari na kyale yaliyo nchi za nje.
Kauli hiyo ilitolewa hivi
karibuni na mwenyekiti wa mfuko wa fursa sawa kwa wote(EOTF),Mama Anna
Mkapa wakati alipotembelea kikundi cha akina mama cha Engiterata Sidai
kilichopo kijiji cha Olgilai wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Akiongea mara baada ya
kuangalia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na kikundi hicho,Mama Mkapa
aliwataka wanakikundi hao kujikita kuzalisha bidhaa zilizo na ubora ili
ziweze kupata masoko ya ndani na nje ya nchi.
Alisema kuwa biashara siku
hizi ni ushindani hivyo wao hawana budi kuzalisha bidhaa zitakazo uzika
sokoni sanjari na kupanua masoko yao.
Akikagua shughuli za
wanakikundi hao ikiwa ni pamoja na mradi wa ngombe wa maziwa sanjari na
kuku wa mayai Mama Mkapa aliwataka wanakikundi hao kutopenda vitu vya
bure katika shughuli zao kwa kuwa mafanikio yanakuja kwa
kujishughulisha.
Hatahivyo,alisisitiza kuwa
yeye pamoja na mfuko wake watasaidia kuwapa elimu ya masuala ya
usimamizi wa fedha wanachama wa kikundi hicho mwishoni mwa mwezi huu
sanjari na kuwaunganisha kupata nafasi ya kuonyesha bidhaa zao katika
maonyesho ya Sabasaba mwaka huu.
Awali mwenyekiti wa kikundi
hicho,Janeth Mollel alimweleza mgeni rasmi kwamba wanajitahidi
kutengeneza bidhaa kwa wingi lakini wanakabiliwa na tatizo la
upatikanaji wa masoko ya uhakika.
Mollel,alisema kuwa tatizo la
mtaji mdogo nalo ni changamoto kwao kwa kuwa wanashindwa kupeleka bidhaa
nje ya nchi na kumtaka Mkapa kuwasaidia katika changamoto hizo.
Hatahivyo,mkurugenzi mtendaji
wa mfuko wa fursa sawa kwa wote,Stephen Emmanuel aliwahaidi wanachama
wa kikundi hicho kuwapatia semina ya siku tatu kuhusu masuala ya
usimamizi wa fedha itakayofanyika jijini Dar es salaam ambapo alisema
gharama za malazi na chakula zitagharamiwa na mfuko huo.