Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Friday, April 26, 2013

RC ARUSHA AMTAKA LEMA ASIINGILIE UONGOZI WA CHUO CHA UASIBU

gari la lema

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Mbunge wa jimbo la arusha mjini Godbless lema ameingia Kitanzini huku akihusishwa na Vurugu za Chuo cha uhasibu Arusha ambapo chuo hicho kwa sasa kimefungwa mara baada ya Vurugu kubwa kuibuka chuoni hapo kwa madai uongozi wa chuo haufuatilii suala la mauji ya wanafunzi wa chuo hicho.
Akiongea na Vyombo vya habari mapema leo mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo alisema kuwa Mbunge  Lema amesababisha vurugu ambazo zililazimu Jeshila polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatanya wanafunzi ambao walitaka kuandamana mara baada ya mwanafunzi mwenzao Hendry Kagu (22)kuuwawa na watu wasiojulikana Juzi.
Magesa alisema kuwa Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vilidai kuwa Mwnaafuzni huyo alichomwa kisu eneo la shingoni lakini wanafunzi walikusanyika kwa madai ya kujadili juu ya kifo hicho na ndipo Lema alipofika na kuaanza kushawishi juu ya wasiwasi wa Kifo hicho.
Aidha ilidaiwa kuwa mara baada ya ushawishi huo ambao pia ulikuwa unadai kuwa mkuu wa chuo anatakiwa kukamatwa ndipo vurugu kubwa sana zilipoibuka ambapo wanafunzi hao walitumia ushawishi wa Lema na kutaka maandamano hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa huku pia wakipanga kudhuru madereva wa Boda boda ambao wangekutana nao.
“Lema alipowashawishi wanafunzi hao wakamkate mkuu wa chuo na pia wafanye maandamano basi  yeye mwenyewe alipiga simu kwa viongozi wa Serikali hapa Mkoani na kudai kuwa hali imechafuka sana huku Uasibu lakini kwa kuwa alikuwa ameshapachika roho ya fujo wanafunzi waliendeleza fujo hizo ambapo tulilazimkika kufika lakini hatukuweza kuvumilia hali hiyo ya vurugu’alisisitiza Magesa.
Pia aliendelea kwa kusema kuwa  alipofika katika eneo lka Tukio akiwa kama Mwakilishi wa Raisi mkoa wa Arusha lakini bado wanafunzi hao hawakutaka kumsikiliza huku wengine wakiendelea kutoa maneno ya kejeli na kuzomea kuwa hawezi kuwasaidia kitu chochote kile
Kutokana na hali hiyo Alidai kuwa Jeshi la Polisi lililazimika kuingilia kati ambapo walitumia mabomu ya machozi kuwatanya maelfu ya wanafunzi ili kurudisha amani kwa muda ndani ya chuo hicho cha uasibu lakini hali haikuwa hivyo.
“nimeshangazwa sana na hii hali ambayo imetokea kamwe wanasiasa kama Lema hawapaswi kuingilia masuala ya Vyuo kwa kuwa kamwe siasa haiwezi kuendana na vyuo lakini kama mbunge anapovuruga amani je nani wa kujenga na kuimarisha amani ya Jiji kama  Lema angekuwa anataka kuwasaidia angeingia kwenye uongozi na wala sio kwenda kwa wanafunzi ‘alibainisha Magesa.
Kutokana na hali hiyo Magesa alisema kuwa  kwa sasa Lema anatafutwa na Jeshi la Polisi lakini pia mpaka sasa baadhi ya Vinara ambao walisababisha vurugu hizo kwa madai kuwa wanamtetea mwenzao Marehemu Hendry wanashikiliwa na Polisi kwa mahijiano zaidi  huku chuo hicho kikiwa kimefungwa kwa muda usiojulikana chini ya Wizara ya Fedha.
Awali akiongelea tukio hilo  Naibu Mkuu wa Chuo hicho cha Uasibu Faraji Kassidi alisema kuwa wamelazimika kufunga chuo hicho ili waweze kutuliza fujo ambayo ingezaa vifo vingi zaidi hivyo kila mwanafunzi anatakiwa kuondoka katika chuo hicho ndani ya masaaa kadhaa.
Faraji alisema kuwa kwa mamlaka aliyopewa anatakiwa kufunga chuo hicho kwa muda usiojulikana ambapo pia uchunguzi wa kifo cha marehemu Hendry bado kinachunguzwa na vyombo vya usalama.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...