Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam Suleiman Kova amesema jeshi hilo
limefanikiwa kukamata silaha nane zikiwemo SMG moja, Pistol tatu, Short
Gun Pump Action mbili, Mark IV moja na Short Gun Greener moja na jumla
ya risasi 27.
Akizungumza
na vyombo vya habari amesema pia wamekamata vipande 12 vya meno ya
Tembo vyenye uzito wa kilogram 47.5 ambapo thamani yake ni shilingi za
kitanzania milioni 36,520,000 na watuhumiwa watatu.
Kamanda
kova amesema kuwa wamekamata magari manne yaliyoibiwa katika maeneo
mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam pamoja na watuhumiwa watano katika
matukio hayo. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni ACP Charles
Kenyela.