Tigo Tanzania imepiga hatua moja nyingine baada ya kuwa
Kampuni ya kwanza Tanzania kuwa Verified katika mtandao wa Twitter. Kabla ya
hapo ni wanasiasa kama Rais Jakaya Kikwete na January Makamba pamoja na watu
maarufu kama Flaviana Matata na Hasheem Thabeet waliokuwa na kialama cha tick
mbele ya majina yao twitter.
Unaweza kujiuliza kuwa verified kwani kuna umuhimu gani,
alama ya tick unayowekewa mbele ya jina lako ni utambulisho unaofanya ueleweke
kwa followers wako kuwa ni wewe na sie mwingine wanaemfahamu. Alama hii hupewa
watu maarufu, makampuni, taasisi na wawakilishi ili kuepusha mkanganyiko
unaotokana na kuwepo kwa parody account. Mpaka sasa zipo account 50,000 tu
zilizokuwa verified dunia nzima.
Nini Faida Yake?