Afisa Mtendaji Mkuu PepsiCo, Asia, Mashariki ya Kati na Africa Bw.
Saad Abdul-Latif akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa SBC Tanzania Bw. Ziad
El Khalil.
Saad Abdul-Latif akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa SBC Tanzania Bw. Ziad
El Khalil.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Bi. Joyce Mapunjo akifurahia jambo na Bw. Saad Adbul-Latif. |
***** ******
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya
vinywaji baridi ya PEPSI kwa Bara la Asia, Mashariki ya Kati na Afrika,
Bw. Saad Abdul Latif, hivi karibuni alifanya ziara nchini Tanzania ikiwa
ni sehemu ya ziara ya kuzitembelea nchi za ukanda wa Afrika Mashariki
(Kenya, Tanzania na Uganda).
Katika ziara hiyo, Bw. Latif, aliambatana na Rais wa Kampuni hiyo ya PEPSI kwa bara la Asia, Mashariki ya Kati na Afrika, Bw. Sanjeev Chadha, ambapo waliweza kukutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Bi. Joyce Mapunjo.
“Ni furaha kubwa kuwa hapa nchini
Tanzania. Kubwa ninaomba muwe na uhaikika ya kwamba Kampuni ya PEPSI,
imedhamiria kuhakikisha kwamba wateja wake wanafurahia bidhaa zenye
ubora wa kimataifa katika bei nafuu zilizo za kirafiki,” alisema Bw.
Latif.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali,
Bi. Mapunjo aliishukuru Kampuni hiyo ya PEPSI kutokana na ahadi yake
iliyojiwekea ya kusaidia katika suala zima la maendeleo ya kiuchumi hasa
katika juhudi zake za kuboresha viwanda, masoko, miundombinu na
usambazaji.
“Kampuni ya PEPSI nchini (SBC Tanzania) inazalisha na kutengeneza nafasi za ajira nchini Tanzania,” aliongeza Bi. Mapunjo.
Hivi karibuni Kampuni ya SBC
imeanzisha kiwanda cha kisasa cha PEPSI katika jiji la Nairobi, ambapo
matokeo yake yamekuwa mazuri naya kutia moyo kutoka kwa wateja. SBC si
tu inatoa chaguo la ziada kwa wateja wake kwenye vinywaji vyake, lakini
pia inatoa thamani ya ziada kwa fedha.
Vinywaji hivi vya PEPSI venye
ujazo wa 350 ML kwenye glasi kinauzwa bei ya kawaida ambayo ni sawa na
bei ya chupa yenye ujazo wa 300 ML. Ni pamoja na Pepsi, Mirinda,
Mountain Dew na aina tofauti za Evervess Kampuni ya SBC Tanzania, ni
kampuni pekee inayozalisha bidhaa mbalimbali za PEPSI nchini Tanzania.