Picha
juu na chini ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
akiwa pamoja na Ujumbe wa Viongozi wa Makampuni ya Maji na Umeme {
Botjheng Water na Megtron } ya Afrika Kusini pamoja Uongozi wa Wizara ya
Ardhi , Makazi, Maji na Nishati aliokutana nao Ofisini kwake Vuga Mjini
Zanzibar.
Mwakilishi
wa Makampuni ya Botjheng Water na Megatron ya Afrika Kusini Bw. Dean
Hiran akiwa pamoja na Viongozi wa Makampuni hayo wakizungumza na
Uongozi wa Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati chini ya Uenyekiti
wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika Picha ya
pamoja na Uongozi wa Makampuni ya Maji na Umeme { Botjheng Water na
Megatron } ya Afrika Kusini mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. Picha
nan Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Uongozi
wa Makampuni yanayojishughulisha na masuala ya Maji Safi na salama ya
Botjheng Water na Megatron kutoka Nchini Afrika Kusini umeamua kutoa
fursa kwa Zanzibar katika uwekezaji wa miradi yao ya Maji na Umeme
ili kuviwezesha Visiwa vya Zanzibar kutekeleza miradi yake ya Kiuchumi
kwa ufanisi.
Mkurugenzi
wa fedha wa Kampuni ya Maji Bw. Hardus Hattingh ameeleza hayo wakati
ujumbe wao ulipokutana kwa mazungumzo na Uongozi wa Wizara ya Ardhi,
makazi Maji na Nishati sambamba na idara zilizohusika na miradi hiyo
chini ya uenyekiti wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi Ofisi kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Bw.
Hardus Hattingh amesema ujio wao Zanzibar ni kuangalia mahitaji halisi
ya Huduma za maji pamoja na kufikiria mbinu zinazoweza kusaidia
kitaalamu kupunguza tatizo hilo.
Mkurugenzi
huyo wa Kampuni ya Maji ya Botjheng Water ya Afrika Kusini amefahamisha
kwamba Kampuni yao imelenga kusaidia Mataifa yenye matatizo ya upungufu
wa huduma hizo wakiangalia zaidi Nchi za Bara la Afrika.
Naye
Mshauri wa Fedha katika Kampuni ya Umeme ya Megatron kutoka Nchi hiyo
ya Afrika Kusini Bw. Johan Oelofse ameeleza kwamba Taasisi yao iko
tayari kuwekeza Zanzibar wakati wowote kutegemea mahitaji
watakayoelezwa.
Bw.
Yohan ameeleza kuwa Kampuni ya Megatron iko tayari na uwezo kamili wa
kuendeleza miradi ya umeme ambayo mengine imeshaanzishwa katika baadhi
ya Mataifa Barani Afrika.
Nao
kwa upande wao Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, makazi, Maji na Nishati
Nd. Al- Khalil Mirza pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Dkt.
Garu wamesema matumizi ya huduma ya maji yataendelea kuongezeka
kufuatia kutanuka kwa sekta ya uwekezaji hapa Nchini hasa katika miradi
ya Utalii.
Wamesema
Mamlaka ya maji inahitaji kuwa na vianzio vingine zaidi vya maji ili
huduma ya maji ifikie katika asilimia ya kiwango kinachohitajika hasa
ndani ya eneo la Mji ambalo bado lina upungufu wa huduma hiyo.
“
Tunaangalia zaidi kuelekeza mipango yetu katika kuhakikisha eneo la Mji
wa Zanzibar ambalo limekabiliwa na idadi kubwa ya wakazi wake
linaondokana na upungufu huo wa huduma ya Maji safi na salama .
Amefafanua Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Dkt.Garu.
Akitoa
shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
amesema juhudi za ziada zinafaa kuchukuliwa katika kuona huduma za maji
safi ndani ya manispaa ya Zanzibar zinapatikana kwa kiwango
kinachoridhisha.
Balozi
Seif amesema Mkoa wa Mjini Magharibi hivi sasa una idadi kubwa ya
wakaazi wake inayofikia Laki 5.9 sawa na asilimia 46% ya wakaazi wote
wa Visiwa vya Zanzibar wapatao Milioni 1.3.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameuomba Ujumbe wa Makampuni hayo ya Maji
na Umeme kutoka Nchini Afrika Kusini kuitumia fursa ya upungufu wa
huduma hizo Zanzibar katika kuwekeza vitega uchumi vyao.