Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Showing posts with label michezo kimataifa. Show all posts
Showing posts with label michezo kimataifa. Show all posts

Sunday, April 20, 2014

MOYES: ROONEY NA FELLAINI WAPO TAYARI KUIVAA EVERTON

                                      
rooney_16d65.jpg
Na Riziki Mashaka.
Kocha Manchester United (David Moyes) amesema kuwa Wayne Rooney na Marouane Fellaini watakwepo katika kikosi cha kwanza kitakachokumbana na Everton siku ya Jumaapili, akiitaja miamba ya mashetani wekundu itaowavaa Everton, Moyes aliwataja Rooney na Fellaini kuwa ni miongoni mwa wachezaji watakaocheza katika mtanange huo.
Fellaini ambaye alikosa mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya katika hatua ya robo fainali dhidi ya Bayern Munich atakuwa fiti kukumbana na Everton wakati Wayne Rooney nae yupo tayari kuibeba ngao ya Man United tayari kupigania ushindi.
Wayne Rooney alishindwa kuonesha makali yake katika mtanange wa klabu bingwa ulaya dhidi ya Bayern Munich baada yakutandikwa mabao 3-1, Rooney aliulimia katika mchezo huo lakini mpaka sasa, Mshambuliaji huyo wa Manchester United yupo tayari kupambana na Everton katika dimba la Goodison Park.

Moyes alisema kuwa Rooney yupo ngangari kwa sasa kwani amefanya mazoezi ya kutosha kwa wiki zima, hivyo atakwepo katika kikosi hicho kitakacho vaana na Everton siku ya jumaapili.
Mskotishi huyo (David Moyes), aliwataja wachezaji ambao bado nimajeruhi kuwa ni Rafael na Rob Van Persie ambao wataukosa mtanange huo wakati akiwataja majeruhi hao, kocha huyo alionesha kuwapa moyo mashabiki wa timu hiyo baada ya kutoa taarifa ya John Evans kuwa atakwepo katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Read More >>

Thursday, January 2, 2014

SOLSKJAER RASMI KOCHA MPYA WA CARDIFF CITY.


 Klabu ya Cardiff City imemtangaza rasmi mshambuliaji wa zamani wa Manchester Utd Ole Gunnar Solskjaer kuwa meneja wao mpya.
Solskjaer ambaye ni raia wa Norway hapo awali alikuwa kocha wa timu ya Molde aliyoiongoza kutwaa mataji mawili ya ligi kuu ya Norway.
Read More >>

Saturday, July 27, 2013

TANZANIA YATOLEWA MICHUANO YA CHAN NA UGANDA

Tanzania (Taifa Stars) imeshindwa kufuzu Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) kwa mara ya pili mfululizo baada ya leo kufungwa mabao 3-1 na Uganda Cranes, hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 4-1.
Stars ambayo ilicheza fainali za kwanza zilizofanyika Ivory Coast mwaka 2009 ilimaliza kipindi cha kwanza katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Kampala ikiwa sare ya bao 1-1.
Wenyeji ndiyo walioanza kufunga bao dakika ya saba katika mechi hiyo iliyochezeshwa na Kanoso Abdoul Ohabee kutoka Madagascar. Frank Kalanda alifunga bao hilo akimalizia mpira uliopigwa ndani ya eneo la hatari la Tanzania.
Bao hilo halikuonekana kuichangaza Taifa Stars, kwani ilitulia na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 18 mfungaji akiwa Amri Kiemba kutokana na pasi nzuri ya Mrisho Ngasa kwenye kona ya eneo la mita 18.
Dakika ya 32 nusura Taifa Stars ipate bao, lakini mkwaju maridadi wa Mrisho Ngasa ambao tayari ulikuwa umempira kipa HAmza Muwonge uligonga mwamba kabla ya kuokolewa na mabeki wa Uganda Cranes.
Mabao mengine ya Uganda Cranes yalifungwa dakika ya 48 kupitia kwa Brian Majwega na lingine dakika ya 63 mfungaji akiwa tenda Kalanda kutokana na makosa ya Salum Abubakar kupokonywa mpira wakati akiwa katika nafasi nzuri ya kutoa pasi kwa mwenzake.
Kocha Kim Poulsen alifanya mabadiliko dakika ya 43 kwa kumuingiza Simon Msuva badala ya Frank Domayo aliyeumia, na dakika ya 78 akawaingiza kwa mpigo Haruni Chanongo na Vincent Barnabas badala ya David Luhende na John Bocco. Hata hivyo mabadiliko hayo hayakubadili matokeo ya mchezo.
Kikosi cha Stars kilipangwa hivi; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, David Luhende/Vincent Barnabas, Aggrey Morris, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Frank Domayo/Simon Msuva, Salum Abubakar, John Bocco/Haruni Chanongo, Amri Kiemba na Mrisho Ngasa.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itarejea nyumbani kesho (Julai 28 mwaka huu) saa 4 usiku kwa ndege ya PrecisionAir.
Read More >>

Mkiambiaji Kenya azirahi uwanjani

                   Cheptai akipewa huduma ya kwanza

Mwanariadha wa Kenya wa mbio za masafa marefu Irine Chebet Cheptai amekimbizwa hospitalini baada ya kuzirai katika mbio za uwanja wa Olimpiki.

Cheptai ambaye alikuwa kuwa mmoja wa wanariadha walioshiriki katika mbio za mita elfu tatu alizirai muda mfupi baada ya kumaliza mbio hizo ambapo alimaliza katika nafasi ya kumi na moja na kuweka muda wake kasi zaidi katika mbio hizo wa dakika nane na sekunde ishirini.
Madaktari waliokuwa uwanjani walimtibu mwanariadha huyo aliyekuwa amepoteza fahamu kabla ya kumkimbiza hospitalini kwa machela.
Ripoti zinasema Cheptai hatimaye alipata fahamu akipokea matibabu hospitalini.
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka ishirini na moja hushiriki katika mbio za mita elfu tano na mwaka huu tayari ameshiriki katika mashindano mawili ya dunia ya IAAF Diamond League.
Mwezi Mei mwaka huu mjini Shanghai, Cheptai aliandikisha muda wa dakika kumi na nne sekunde hamsini nukta tisa tisa, muda ambao ndio bora zaidi aliouandikisha katika mbio hizo.
Read More >>

Wednesday, July 17, 2013

Video: Baada ya shabiki wa Arsenal Vietnam kukimbiza gari la wachezaji kwa zaidi ya KM 5 hatimae apewa shavu lakuingia kwenye gari na kupiga nao picha



Baada ya wachezaji wa Arsenal kudondoka Asia kwenye tour yao ya 2013, wakiwa Vietnam walikutana na kijana ambae iliwalazimu kumpa nafasi ya kupanda kwenye gari lao lililojaa wachezaji pamoja na kocha wa timu hiyo "Wenger" na kupiga nae picha huku wakimshangilia kwa makofi baada ya kukimbiza gari hilo kwa zaidi ya kilometa 5
Read More >>

Tuesday, July 16, 2013

Rudisha hatashiriki mbio za dunia Moscow

David Rudisha wakati wa michezo ya Olimpiki mjini London
Bingwa wa Olimpiki na dunia na mshikilizi wa rekodi ya ulimwengu katika mbio za mita mia nane kwa wanaume mkenya David Rudisha, amejiondoa kutoka kwa mashindano yajayo ya dunia yatakayofanyika mjini Moscow Mwezi Ujao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, na naibu makamu wa rais wa shirikisho la mchezo wa riadha nchini Kenya, David Okeyo, Rudisha hatalitetea taji lake mwaka huu kutokana na jeraha.
Okeyo amesema baada ya kushauriana na mwanariadha huyo pamoja na makocha wake, imebainika kuwa Rudisha bado angali anauguza jeraha na haitakuwa vyema kwake kushiriki katika mashindano hayo kwa kuwa inaweza kuhatarisha zaidi jeraha hilo.
''Nasikitika sana kuwa siwezi kuteteza taji langu la mita mia nane mjini Moscow. Jeraha langu la mguu halijapona kwa wakati ufaao ili kuniwezesha kushiriki katika fainali hizo za dunia. Kwa hivyo nawatakia wanariadha wenzangu kila la heri katika mashindano hayo ya dunia yatakayofanyika mjini Moscow.'' Amesema Rudisha.
Maelezo zaidi baadaye.

Chanzo: BBC Swahili
Read More >>

Friday, July 12, 2013

Neymar hatarini kuburuzwa Kortini.

Barcelona-Neymar-2013-HD-Wallpaper-1280x720
Kampuni ya masuala ya masoko ya michezo  DIS ambayo pia  inamiliki supermarket nchini Brazil imetishia kumburuza nyota wa Brazil aliyesajiliwa na klabu ya Barcelona hivi karibuni Neymar kwa kile ilichokiita kudhulumiwa haki yake katika mauzo ya mchezaji huyo .
DIS inadai kuwa ilikuwa inamiliki haki za Neymar kwa asilimia 40% na ilikuwa na haki ya kupata fedha kwenye mauzo ya mchezaji huyo lakini hadi sasa hakujawa na mawasiliano yoyote baina ya kampuni hiyo na wawakilishi wa Neymar hali inayowafanya kuwa na wasiwasi wa kupata haki yao.
Kwa mujibu wa mahojiano maalum yaliyofanywa baina ya kiongozi wa kampuni hiyo na kituo cha habari cha Marekani cha Bloomberg , DIS inapaswa kulipwa fedha kutokana na Euro milioni 57 ilizolipwa Santos baada ya kumuuza Neymar , pamoja na Euro Milioni mbili kama Neymar akichaguliwa kuwa mmoja wa wachezaji watatu wanaowania tuzo ya Mchezaji bora wa dunia ya Ballon D’or pamoja na fedha nyingine zaidi zitakazotokana na mazuo ya tiketi kwenye mechi mbili za kirafiki baina ya Santos  na Barcelona ambazo ni sehemu ya makubaliano ya mauzo ya mchezaji huyo ambapo kama mechi hizo hazitachezwa Barcelona italazimika kulipa fidia ya Euro milioni 4.
Kampuni hiyo imesema kuwa itafanya mazungumzo na Santos kabla ya kuchukua hatua za kisheria ambapo itawashitaki Barcelona pamoja na Neymar mwenyewe kwa kukiuka makubaliano ya kimkataba .
Barcelona ilimununua Neymar kwa Euro Milioni 57 ambapo ripoti kadhaa zimedai kuwa Santos imeambulia Euro Milioni 9 pekee kwenye mauzo hayo huku fedha nyingine zikienda kwa makampuni kadhaa na watu binafsi ambao walikuwa wanamiliki sehemu au asilimia za haki za mchezaji huyo .
Utata huu kwenye mauzo ya Neymar unatokana na Umiliki wa mtu wa tatu ambao umezoeleka kwenye bara la Amerika ya kusini ambako mara kadhaa watu binafsi na makampuni humiliki sehemu ya haki za wachezaji hali ambayo mara nyingi huleta utata pale mchezaji husika anapouzwa .neymar-barcelona-salary-million-euros
Read More >>

PAMOJA NA KUFUNGWA 6 - 1 NA MAREKANI - WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA BELIZE WASEMA WALIKATAA RUSHWA YA $13000 YA KUPANGA MATOKEO


Kufuatia kipigo cha cha 6-1 kutoka kwa United States katika mechi yao ya kwanza ya makundi kwenye michuano ya Gold Cup,  wachezaji wengi wa kikosi kilichoanza cha timu ya taifa ya  Belize wamesema kwamba walifuatwa kwa ajili ya kupewa rushwa ili kupanga matokeo ya mchezo huo. Belize, ambao wapo katika mpango wa kukusanya kiasi cha $25,000 zinazotakiwa kwa ajili ya kuhudumia safari zao ndani ya USA wakati wa michuano hiyo, walifunga bao lao la kwanza kwenye dakika ya 40 ya mchezo baada ya Chris Wondolowski kuwafungia wenyeji mabao mawili ya kuongoza katika dakika ya 12 na 37. Wondolowski baadae akaongeza bao la 3 kabla ya mapumziko na wachezaji wenzie wakaongeza mengine matatu katika kipindi cha pili, bao mja likifungwa na Landon Donovan kwa penati katika dakika ya 76.
Wachezaji wa Belize wamesema kwamba waliataa hongo ya kiaisi cha €10,000($13,074) kwa kila mchezaji — wakitaka kulinda heshima ya nchi yao.
"(Mtoa rushwa) alianza kutuambia kwamba hatuna nafasi ya kuwafunga Marekani hivyo alitaka atupe kiasi cha pesa ili tubadilishe maisha yetu huko nyumbani Belize lakini tufanye atakavyo yeye kwenye mchezo dhidi ya Marekani," Mlinzi wa Belize Ian Gaynair aliiambia 7 News Belize.
Wachezaji hao wanasema walifuatwa kwa mara ya kwanza wakati wakiwa kwenye uwanja wa ndege wa Guatemala kabla ya kukutana tena na mtu huyo kwenye shopping mall ya Portland.
"Nilimuelewesha kwamba hatukuhitaji fedha zake kutoka kwake, na tulikuwa US kwa ajili ya kulinda heshima ya nchi yetu na sio vinginevyo," alisema golikipa wa Belize Woodrow West.
Read More >>

Thursday, July 11, 2013

MKONGWE KOLO TOURE AMTAKA SUAREZ KUBAKIA LIVERPOOL ASHINDE MATAJI, ASIFIA MIPANGO YA MAJOGOO HAO WA JIJI!!

Opportunity: Kolo Toure has said that it will be a challenge to replace Jamie Carragher in Liverpool's defence
  Shavu kubwa: Kolo Toure alisema ni changamoto kubwa sana kurithi mikoba ya beki mkongwe Jamie Carragher katika klabu yaLiverpool
 
Wakati mshambuliaji nyota wa majogoo wa jiji ama wekundu wa Anifield, klabu ya Liverpool, raia wa Uruguay, Luis Saurez akiendelea kusisitiza nia yake ya kutaka kuondoka klabuni hapo kwa madai ya kutaka kucheza UEFA,  beki mpya wa miamba hiyo ya soka, Kolo Toure amemuambia kuwa anaweza kutimiza ndoto zake kwa kuichezea klabu hiyo kwani benchi la ufundi lina mipango mizuri sana ya kuifikisha mbali.
 
Toure beki wa zamani wa The Gunners, Asernal amesema nia ya Suarez ni nzuri sana, lakini ajua huko anakotaka kwenda mambo yanaweza kuwa magumu afadhali Liverpool, hivyo abaki na kuisaidia timu ili ipate mafanikio makubwa siku zijazo.

Lakini ikumbuke kuwa Toure mnamo mwaka 2009 aliihama Asernal na kujiunga na Manchester City kwa sababu inayofanana na ya Suarez, ila kwa sasa amemshauri nyota huyo raia wa Uruguay kuendelea kuichezea Liverpool ili aonje mafanikio yajayo siku za usoni.

 
Raring to go: The Liverpool players were training this week at their Melwood Training Ground 
Liverpool wanaendelea na mazoezi wiki hii katika uwanja wao wa mazoezi wa Melwood 
“Kiukweli Luis kama atakubali kubaki, ana nafasi ya kushinda mataji mengi”, alisema Toure. 

klabu hii inaandaliwa kwa mafanikio, umoja, mpangilio wa mambo kwa viongozi na morali ya wachezaji, ni dalili ya kuijenga upya timu hii, hivyo vyema Luis akabakia.

Toure alisema Liverpool ni timu kubwa sana. Luis ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa, ana vitu vingi vya uwanjani. Lakini klabu ndio yenye uwezo wa kufanya maamuzi ambayo yatakuwa mazuri kwa kila mtu.

Nyota huyo raia wa Ivory Coast, ni mchezaji mpya aliyesajiliwa katika majira haya ya joto ya usajili barani Ulaya  akitokea Man City alikomaliza mkataba wake, na amepewa nafasi hiyo kuziba pengo la Jamie Carragher aliyetangaza kustaafu soka. 

Plea: Luis Suarez, seen here playing for Uruguay at the Confederations Cup, is keen to leave Liverpool  
Staa wa ukweli: Luis Suarez, hivi karibuni alionekana katika michuano ya kombe la Mabara nchini Brazil akiichezea timu yake ya taifa ya Uruguay, na sasa ametangaza nia ya kuihama Liverpool
 
Premier League veteran: Kolo Toure moved from Manchester City to Liverpool 
Mkongwe wa ligi kuu England: Kolo Toure ameihama Manchester City  na kujiunga na Liverpool huku akikabidhiwa jezi namba 4
 
“Ni heshima kubwa kuichezea Liverpool,” alisema Toure. “Nimekaa hapa kwa wiki mbili na kuona mambo mengi mazuri. Nitatoa mchango wote kwa klabu ya Liverpool.  Jamie Carragher alikuwa mchezaji muhimu sana na Liverpool wanahitaji mtu wa kuziba pengo lake. Hii ni klabu ya makombe. Nataka kuwa sehemu ya Historia klabuni hapa.”
Read More >>

ARSENAL YAJIPANGA KUMSAJILI FABREGAS KWA DAU LA PAUNI MILIONI 25, KUUMIA KWA VERMAELEN KWAWACHANGANYA, WAMFUKUZIA BEKI WA SWANSEA

 Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Washika bunduki wa kaskazini mwa jiji la London, klabu ya Arsenal, wamefufua upya mipango ya kutaka kumsajili na kumrudisha tena London nahodha wao wa zamani na mwanandinga wa wazee wa Katalunya kwa sasa, FC Barcelona, namzungumzia kiungo  Cesc Fabregas katika majira haya ya joto.
Nyota huyo wa zamani wa Asernal kwa sasa yupo mapumzikoni akila raha na kuweka akili sawa kufuatia kuwa na msimu mgumu Camp Nou na anapumzika baada ya kumaliza majukumu ya kuitumikia timu yake ya taifa ya Hispania iliyoshindwa kutwaa kombe la mabara baada ya kufungwa na wenyeji Brazil mabao 3-0 katika mchezo wa fainali.Taarifa za huko Hispnia zinadokeza kuwa nyota huyo bado ana nia ya kubakia Camp Nou, lakini bado wasiwasi umetanda kama ataendana na mipango ya kocha Tito Vilanova, na ikizingatiwa kuwa msimu uliopita alikaa benchi katika baadhi ya mechi kubwa kwa klabu yake.

 Hana furaha? Maisha ya Cesc Fabrega katika klabu yake ya Barcelona yameenda tofauti na mipango yakeEndapo kiungo huyo ataamua kutoka, Asernal hawatapata shida kumrudisha kwani wakati wanamuuza kwa pauni milioni 25 kwenda Barca, kulikuwa na makubaliano kuwa endapo Fabregas mwenye umri wa miaka 26 atakuwa anaihama klabu hiyo, The Gunners watakuwa wa kwanza kufikiriwa.
Kama Wakatalunya watamuuza Fabregas, washika bunduki wa London watakuwa wakwanza kumrejesha nahodha wao kwa usajili wa pauni milioni 25
 Hashawishiki?  Bosi wa Barca Tito Vilanova amempotezea Fabregas katika michezo mingi muhimu
Wakati huo huo, washika bunduki wa London wameamua kufufua mipango yao ya kumsajili beki wa Swansea,  Ashley Williams kufuatia  Thomas Vermaelen kurejea katika majeruhi.
Nyota huyo wa Wales anawindwa sana na  Arsene Wenger majira haya ya usajili, lakini wameshindwa kufikia dau linalohitajika la pauni milioni 10.
Mtandao wa michezo wa Sportsmail.com ulisema jumanne ya wiki hii kuwa, nahodhaVermaelen atakosa maandalizi ya msimu mpya kutokana na majeruhi, na ataiacha Arsenal ikiwa na mabeki wazima wawili wa kati; Laurent Koscielny na Mertesacker. 
Majeruhi ya  Thomas Vermaelen yanawalazimu Arsenal kuanzisha mbio za kumsaka Ashley Willia 
FULL SHANGWE
Read More >>

Bayern Munich na Manchester United wagombania saini ya Thiago

Ppe Guardiola ametangaza kumtaka Thiago ndani ya Bayern Munich

Huku tetesi nyingi za vyombo vya habari zikidai kuwa dili la usajili wa nyota wa timu ya taifa ya Hispania chini ya Miaka 21 kwenda Manchester United limekamilika Bayern Munich wamejitokeza na kutangaza wazi nia ya kumsajili nyota huyo hali inayofanya kuwepo kwa vita kali baina ya Wajerumani (Munich) na Waingereza (Man United) kuwania sahihi ya nyota huyo (Thiago Alcantarra) .

Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola akizungumza na waandishi wa habari hii leo amesema kuwa anamfahamu vizuri Thiago na angependa kumsajili kwa kuwa ana uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya nne au tano .

Guardiola amesema kuwa kwa sasa mchezaji ambaye angependa kumsajili ni Thiago na kama hataweza kushawishi kujiunga na Bayern basi hatasajili mchezaji mwingine . Kauli hii ya Guardiola inamaanisha kuwa timu hizo mbili za United na Bayern kwa sasa zitakuwa zikihaha kila moja ikijaribu kumshawishi nyota huyo kusaini kwenye timu mojawapo.


Thaigo ndio ataamua kwenda United au Bayern Munich

United kwa muda mrefu wamekuwa wkaitajwa kuwa mbioni kumtangaza mchezaji huyo kama mchezaji wa kwanza mwenye jina kubwa kusajiliwa na David Moyes baada ya usajili wa beki wa Uruguay Guillermo Varella na kiungo huyo (Thiago) amekuwa akijaribu kuondoka Barcelona ambako ameshindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza .

Thiago Alcantarra ana malengo ya kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya taifa ya Hispania kwenye michuano ya kombe la dunia huko nchini Brazil mwakani na amekuwa akipambana kuondoka Barcelona ili aende mahali ambako atamshawishi kocha Vicente Del Bosque kumpa nafasi . Mkataba wa Alcantara unaonyesha kuwa asipocheza kwenye asilimia 60% ya mechi za timu hiyo anaweza kuuzwa kwa bei ya Euro Milioni 18 na kwa msimu uliopita hakucheza kwa kiwango hicho hali inayofanya kuondoka kwake kuwa rahisi .

David Moyes ataipata saini ya Thiago au United watapigwa bao na Bayern Munich
Read More >>

ANGALIA PICHA ZA MAPOKEZI YA TIMU YA MAN UNITED

Arrival: Manchester United landed in Bangkok as they prepare to get their pre-season underway
Wanawasili: Manchester United wamewasili Bangkok kujiandaa kwa msimu mpya
Rio Ferdinand
Wayne Rooney
Sare sare: Rio Ferdinand (kushoto) na Rooney kulia
Arrival: Manchester United landed in Bangkok as they prepare to get their pre-season underway
NA BIN ZUBERY.
Flashpoint: The United squad was bombarded with cameras as they land in Bangkok
kamera kamera: Kikosi cha United kilipokewa na kamera kilipotua Bangkok
Girls just wanna have fun: Manchester United fans welcome the players as they land in Thailand
Vimwana sasa: Mashabiki wa Manchester United wakiwakaribisha wachezaji wao walipotua Thailand
Manchester United fans welcome the players as they land in Thailand
New beginnings: David Moyes will get his first look at his new charges after taking over at United
New beginnings: David Moyes will get his first look at his new charges after taking over at United
Mwanzo mpya: David Moyes ataanza kazi rasmi baada ya kuchukua mikoba ya ukocha United
Tribute: Moyes pays respect to the monarch at Siriraj Hospital in Bangkok ahead of United's tour
Moyes akiwa katika hospitali Siriraj mjini Bangkok 
Respect: Moyes and Ryan Giggs stand next to the image of Thai King Bhumibol Adulyadej and Queen Sirikit
Heshima: Moyes na Ryan Giggs wakiwa wamesimama pembeni ya picha za Mfalme wa Thai, Bhumibol Adulyadej na Malkia Sirikit
Welcome: The United squad are greeted by passionate fans in Bangkok
Karibu: Kikosi cha United kimepokewa vizuri Bangkok
Welcome: The Manchester United squad are greeted by passionate fans in Bangkok
Karibuni: Manchester United walivyopokewa Bangkok
Smile for the camera: Rio Ferdinand ensures he'll have plenty of memories from the trip to Thailand
Tabasamu la kamera: Rio Ferdinand akipiga picha za video Thailand
Wilfried Zaha
Manchester United football player Ryan Giggs
Wakongwe: Ferdinand (kushoto) na Ryan Giggs kulia

Read More >>

Tuesday, July 9, 2013

Brazil: Refa auwawa na kukatwa kichwa na mashabiki baada ya kumchoma kisu na kumuua mchezaji. tunaomba radhi kwa video hii kama itakukwaza


Refa Otavio Jordao da silver (20) kutoka brazil auwawa kikatili na kunyofolewa kichwa baada ya kumchoma kisu na kumuua mchezaji Josenir Dos Santos Abreu (30) uwanjani katika mechi ya kienyeji iliyofanyika June 30. Moranhao, Brazil.
 inasemekana refa huyo aliingia katika ubishani na mchezaji Josenir baada ya kupuliza kipenga. baada ya kushindwana katika ubishi huo, refa alichukua kisu cha mfukoni na kumchoma mara nyingi na kusababisha kifo cha mchezaji huyo ambae alifia njiani akikimbizwa hospitali.
Baada ya tukio hilo watu walio na hasira na wanao aminika kuwa ndugu na marafiki wa mchezaji huyo, walimshambulia refa huyo, wakaanza kumpiga, wakamfunga na kumpiga na mawe kabla ya kumkata kichwa na kukitundika kwenye mti na baadae kukisimika katikati ya uwanja.
Mpaka sasa polisi wanamshikilia Luiz Moraes de souza (27) kwa tuhuma za mauaji hayo, ambae amekubali kumtukana refa huyo lakini amekanusha kumuua
Read More >>

Monday, July 8, 2013

CAMERON, MALKIA WAMPONGEZA MURRAY KWA KUIPA HESHIMA UINGEREZA.

WAZIRI Mkuu David Cameron na Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza wamekuwa miongoni mwa watu mashuhuri waliotoa pongezi kwa mchezaji tenisi nyota wan chi hiyo Andy Murray kwa kunyakuwa taji la michuano ya Wimbledon. Wachezaji nyota na watu wengine maarufu nchini humo pia walitoa pongezi zao kwa Murray mwenye umri wa miaka 26 baada ya kuwa Muingereza wa kwanza kunyakuw ataji la michuano hiyo toka Fred Perry alipofanya hivyo mwaka 1936, kwa kumfunga Novak Djokovic kwa seti 3-0. 

Cameron ambaye alikuwepo uwanjani kushuhudia mtanange huo alimpongeza Murray kwa kuonyesha kiwango cha juu kwenye mchezo huo na kuweka historia mpya katika mchezo huo nchini Uingereza. Mwandishi wa BBC katika kasri ya kifalme nchini humo, Peter Hunt alibainisha kuwa Malkia alimtumia ujumbe binafsi Murray kumpongeza kwa kufanikiwa kushinda taji hilo.
Read More >>

BOLT ASHINDA MBIO ZA DIAMOND LEAGUE ZA PARIS.

.


MWANARIADHA nyota wa mbio fupi kutoka Jamaica, Usain Bolt ametuma ujumbe kwa wapinzani wake baada ya kufanikiwa kushinda mbio za mita 200 za Diamond League zilizofanyika jijini Paris kwa kutumia muda wa sekunde 19.73 ukiwa ni muda wa haraka zaidi kwa mwaka huu. Bolt ambaye anashikilia rekodi ya dunia katika mbio hizo alifabnikiwa mbio kirahisi na kuuzidi muda wa haraka zaidi uliowekwa kwa mwaka huu na Tyson Gay wa Marekani mwezi mmoja kabla ya mashindano ya riadha ya dunia yatakayofanyika jijini Moscow, Urusi. Akihojiwa mara baada yam bio hizo Bolt amesema anajisikia vyema kwa kushinda mbio hizo lakini bado bado ana kazi ya kufanya kuhakikisha anakuwa katika kiwango chake ifikapo michuano ya dunia. Nafasi ya pili katika mbio hizo ilikwenda kwa Warren Weir wa Jamaica aliyetumia muda wa sekunde 19.92 huku nafasi ya tatu ikienda kwa Christophe Lemaitre wa Ufaransa aliyetumia muda wa sekunde 20.07.

Read More >>

Friday, July 5, 2013

BREAKING NEWS: MOYES ASEMA: ROONEY HAUZWI, ATAENDELEA KUWA MCHEZA WA UNITED - KUHUSU RONALDO ASHINDWA KUKATAA WALA KUKUBALI KUTAKA KUMSAJILI


Kocha wa Manchester United David Moyes leo hii amethibitisha kwamba mshambuliaji wa klabu hiyo Wayne Rooney hayupo sokoni na ataendelea kuicheza klabu hiyo kwa mingi ijayo.

Akizungumza kwenye mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu ajiunge na klabu hiyo akichukua nafasi ya Sir Alex Ferguson, Moyes alisema:"Nimeongea na Wayne Rooney. Wayne yupo nyuma ya mabao 40 kumfikia Sir Bobby na Denis Law. Wayne hauzwi - ni mchezaji wa Manchester United - na ataendelea kubakia kuwa mchezaji wa Manchester United. Nimekuwa na mikutano nae kadhaa. Amerudi kwenye hali nzuri na anafanya vizuri mazoezini. Tunajaribu kufanya kila kitu kumrudisha Wayne Rooney kuwa kama alivyokuwa zamani - Wayne Rooney ambaye tunamjua.

"Vyovyote vilivyotokea kabla, tunafanya kazi pamoja sasa. Macho yake yanaonyesha ni mtu mwenye furaha, ni lazima niseme Wayne hauzwi. Kuliwahi kuwepo mkutano wa siri baina ya Rooney na Sir Alex. Mie naendelea mbele sasa, sijui nini kilizungumzwa kwenye mkutano huo. Ninachofikiria sasa ni kusonga mbele na kufanya kazi ya kumrudisha Wayne Rooney kwenye ubora wake. "

Alipoulizwa kuhusu Cristiano Ronaldo, Moyes alijibu: "Sitomzungumzia yeye moja kwa moja na wachezaji wengine wa vilabu vingine. Lakini hii klabu siku zote imekuwa ikivutiwa na wachezaji bora duniani."

Pia Moyes alithibitisha kwamba winga mpya wa klabu hiyo aliyesajiliwa kutoka Crystal Palace - Wilfred Zaha ambaye amekuwa akiwindwa na vilabu vingi kujiunga navyo kwa mkopo - Moyes amesema mchezaji huyo ataungana na Manchester United kwenye tour ya pre-season, kama ilivyo kwa wachezaji wengine. 

Wakati huo huo alipoulizwa kuhusu usajili wa wachezaji wapya, Moyes amesema angependa kusajili wachezaji mapema lakini mambo yamekuwa yakichelewa kutokana na makocha ambao ndio wanaothibitisha uuzwaji wa wachezaji wengi wamekuwa likizo au ndio wanaingia kwenye vilabu vyao vipya.
Read More >>

Monday, July 1, 2013

ROONEY KUBAKI AU KUONDOKA MAN UNITED ITAJULIKANA KESHO BAADA YA KIKAO CHAKE NA MOYES


Big contract: Wayne Rooney will discuss his future as Arsenal and Chelsea wait


KOCHA David Moyes anajiandaa kukutana na Wayne Rooney na wawakilishi wake kwa mazungumzo kesho, hilo likiwa jukumu lake la kwanza kubwa tangu aanze kazi Manchester United.

Mkataba wa miaka sita wa Mscotland huyo umeanza rasmi leo na atakwenda makao makuu ya klabu, Carrington kutatua sakata la muda mrefu la Rooney kutaka kuondoka.

Moyes anataka Rooney abaki, lakini anafahamu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 25.6 mwaka 2004 anataka kuondoka.


Shake it off: Wayne Rooney was at Glastonbury music festival over the weekend
Tingisha: Wayne Rooney alikuwa kwenye tamasha la muziki Glastonbury mwishoni mwa wiki


Under new management: Moyes is considering the future of Rooney at Old Trafford
Chini ya utawala mpya: Moyes anashikilia mustakabali wa Rooney Old Trafford

 

Inafahamika mwanasoka huyo wa kimataifa wa England amejenga fikra zake kwamba kubadilisha klabu ni njia nzuri kufufua makali yake kuelekea Fainali za Kombe la Dunia majira yajayo ya joto.

Zaidi itategemea na mazungumzo yake na Moyes ambaye anafanya jitihada za kumbakiza.

Arsenal na Chelsea zote zinamfuatilia na zina ya kumsajili Rooney na ikiwa United itakubali kumuuza watalazimika kumuacha ajiunge na moja ya wapinzani wao katika Ligi Kuu England.

Kama Rooney atataka kuondoka, United pia inaweza ikataka ada ya uhamisho ya kiasi cha Pauni Milioni 35, ambazo  Paris Saint-Germain na Real Madrid zinaweza kutoa kununua huduma ya mpachika mabao huyo.

Kocha wa Real, Carlo Ancelott ni shabiki wake, lakini kumfikiria Rooney itategemea na Mtaliano huyo mipango yake ya kuwasajili Luis Suarez wa Liverpool na Edinson Cavani wa Napoli itakuwaje. 

Arsenal wako tayari kuvunja rekodi yao ya usajili na kumfanya pia Rooney awe mchezaji anayelipwa zaidi kwa kiasi cha mshahara wa Pauni 170,000 kwa wiki, ambacho ni cha chini kutoka Pauni 225,000 anazolipwa kwa sasa. 

Moyes anatakiwa kumaliza suala hili mapema ikiwa anataka kumpata mbadala sahihi. 

Aatashughulikia nyongeza ya dau la kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Everton, Leighton Baines Pauni Milioni 15 na mazungumzo rasmi na Barcelona kuhusu usajili wa Pauni Milioni 17 wa kiungo Thiago Alcantara. 


Mkataba mkubwa: Wayne Rooney atajadili mustakabali wake huku Arsenal na Chelsea zikimsikilizia


Bayern Munich, Manchester City na Real Madrid nazpo zinafuatilia pia sakata hilo. Monaco itamfuata Patrice Evra iwapo dili la Baines litakamilika na timu hiyo ya Ufaransa pia bado inamtaka winga Mreno wa United, Nani. 

Kadhalika, suala la AC Milan kutaka kumsajili Nemanja Vidic limetupiliwa mbali na wakala wake,  Silvano Martina aliyesema: "Vidic hana tatizo United, yanayozungumzwa yote ni uvumi,".

Wakati huo huo, Arsenal ofa yake ya Pauni Milioni 6 kwa kiungo wa Lyon, Clement Grenier, mwenye umri wa miaka 22 imepigwa chini.
CREDIT: bIN ZUBEIRY BLOG
Read More >>
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...