Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Showing posts with label filamu. Show all posts
Showing posts with label filamu. Show all posts

Thursday, August 15, 2013

Hatimaye Muigizaji Elizabeth Michael (Lulu) arejea kazini, anazindua movie yake ya kwanza tangu kutoka jela tarehe 30 August

Muigizaji Elizabeth Michael (LULU) anatarajia kuachia movie yake ya kwanza tangu alipotoka jela "Foolsh Age" siku ya tarehe 30 mwezi wa nane katika ukumbi wa Mlimani City huku kukiwa na wasanii wa muzini pamoja na Jay Dee na Machozi Band ambao watasindikiza uzinduzi huo.


hotlulumichaelNina kila sababu ya kumshukuru Mungu....!!!ninafuraha ya kuwafahamisha kuwa TAREHE 30/8/2013 ndio siku nitakayozindua movie ya mpya ya FOOLISH AGE....hatimaye narudi kazini!!!!Uzinduzi utafanyika katika ukimbi wa MLIMANI CITY....kutakuwepo na wasanii mbalimbali wa muziki....na pia LADY JAY DEE pamoja na MACHOZI BAND atakuwepo pia!!!nahitaji support ya mashabiki wote wa LULU na mashabiki wa BONGO MOVIE.....♥♥♥♥!!!#PROINPROMOTERS
Read More >>

CHEKI JIMMY MASTER NA HEKA HEKA ZA UJIO MPYA WA DOBLE J FINAL

Jimmy Master

YULE muongozaji na mwigizaji Jimmy Mponda 'Jimmy Master' aliyetikisa  na mfululizo wa filamu za misuko iliyotoka sehemu ya kwanza hadi ya tatu na baadaye kujiongezea jina lingine akiitwa J Plus.
 
Kwa sasa nyota huyo amefunguka  kuwa yukombioni kutoa muvi ya mwisho inayoitwa Doble J Final  huku ujio huo ukiwa ni wa mwisho kutoka baada ya kutangulia  na Doble J sehemu ya kwanza na yapili zilizotoka mwaka jana.

"Mwaka jana nilifanikiwa kukonga nyoyo za mashabiki wa filamu hususani  wanaopagawa na filamu za mapigano na kujawa mambo ya  kipelelezi,"alisema J Plus.

Alisema Doble J Final pia ni ujio wake wa filamu nyingine ya mapigano na  kuna heka heka za kipelelezi ndani. J Plus aliyezoeleka sasa katika kuonesha ubabe wa kufa mtu , kwa sasa ujio wake huo unao tazamiwa kuingia sokoni mapema tu , mwezi ujao . 
 
Pia Jimmy Master amemshirikisha mbabe mwingine katika filamu za mapigano Ibrahim Mbwana  'Bad Boy' na pia wamo nyota wengine katika dulu la filamu kama Charles Magari , Hashim Kambi na Veronica Viankero.
Read More >>

DKT. FENELLA AKUTANA NA WADAU WA FILAMU NA KUZUNGUMZA NAO.

PIX 1 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Waziri Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na Viongozi wa Steps (hawako pichani) wakati walipomtembelea ofisini kwake kwa mazungumzo juu ya maendeleo ya kazi za sanaa jijini Dar es Salaam.
PIX 7 
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bi. Joyce Fissoo akichangia wakati wa kikao kati ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara na Steps.

…………………………………………………………………

Na Benedict Liwenga-MAELEZO
WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara amekutana na wadau wa Kampuni ya Steps Entertainment  na kuzungumza nao juu ya maendeleo ya Tasnia ya Filamu nchini. Ujumbe huo wa Steps ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu Bw. Dileshi Solanki.

Katika mazungumzo hayo Dkt. Fenella amegusia masuala ya uharamia katika kazi za filamu nchini na kutia mkazo katika suala zima la maadili. Aidha Waziri ameeleza kuwa kuanza kwa urasimishwaji wa tasnia ya filamu na muziki unaoendelea kutekelezwa nchini kutasaidia sana kuondosha kazi zisizohalali. 

Aidha, Dkt. Fenella amewashauri wadau  wa tasnia ya filamu nchini washirikiane kikamilifu na Serikali katika kuendeleza na kukuza tasnia ya filamu na pia kuhakikisha wasanii wananufaika na jasho lao. Aidha ameeleza umuhimu wa kutoa elimu kwa wadau na umma kwa ujumla juu ya fursa nyingi zilizopo katika tasnia.

Kwa upande mwingine Waziri Dkt. Fenella ameshauri pia kuwe na majumba maalum kwa ajili ya kuonyeshea sinema ambayo yatakuwa yanazipa kipaumbele filamu za kitanzania pia amehamasisha wadau wa filamu kuanzisha majumba hayo na ambao tayari wameanzisha kutoa fursa hiyo ili kuziendeleza kazi za filamu za kitanzania.

“Kuwe na majumba ya kuonyeshea sinema ambayo yatakuwa yanazipa kipaumbele filamu za kitanzania”. Alisema Dkt. Fenella.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo alibainisha kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la filamu zinazowasilishwa kwa ukaguzi na pia wadau wameanza kutumia stempu za TRA katika kazi za filamu na muziki ili kuzilinda kazi hizo. 

Stampu zilianza kutolewa tangu mwezi Januari mwaka huu .

Kwa upande mwingine Mkurugenzi Mkuu Bw. Dileshi Solanki wa Kampuni ya Steps Entertainment ameiahidi Serikali kupitia Waziri wa Habari, Vijana na Utamaduni na Michezo Mhe Dkt Mukangara, kuendelea kuendeleza tasnia ya filamu kwa kushirikiana kikamilifu na serikali na kupiga vita uharamia dhidi ya filamu za kitanzania . Aidha wameiomba serikali kuendelea kuwajengea mazingira mazuri.
Read More >>

Saturday, July 27, 2013

KAMPUNI ZA NJE ZAANZA KUVUTIWA KUSAMBAZA FILAMU ZA KISWAHILI.


Muigizaji mmoja maarufu nchini ambaye kwasasa yupo nje ya nchi amesema kuwa katika safari yake hiyo nje ya nchi moja ya vitu anavyofanya ni kushawishi na kuzungumza na baadhi ya kampuni za nje ili kuweza kuwekeza nchini katika tasnia ya filamu hasa katika usambazaji ambao kwasasa unadaiwa kuwepo kwa kuangalia jina la star aliyepo ndani ya filamu husika au ukaribu wa msanii na msambazaji pasipo kuangalia ubora wa kazi zikiwemo kutoka kwa waandaaji na wasanii chipukizi. "nimeshaongea na kampuni moja wanataka kufanya hivyo kwa kusambaza nchi tofauti pamoja na Tanzania na ndiyo wanataka kuanza kwa hiyo naona itakuwa vizuri ngoja tuone" alisema msanii huyo akiongea na Swahiliworldplanet.

Kuhusu wasanii wa Tanzania kuanza kusambaza kazi zao kupitia katika mitandao kama baadhi ya nchi zilizoendelea msanii huyo alisema "  kuuza net pia bongo imeanza wanafanya steps nasikia lakini bado itakuwa faidia yao siyo ya wasanii kama msanii unamuuzia kazi nzima huwezi kuhusika kwenye hayo mauzo"
Kwasasa bado kuna kampuni chache za kusambaza kazi za wasanii nchini na pia inadaiwa kuna msambazaji mmoja anawafanyia wenzake hujuma ili abaki yeye pekee katika kusambaza kazi za wasanii.
Uwepo wa kampuni nyingi za usambazaji utachochea ushindani katika kusambaza kazi za wasanii na hata malipo yao kuongezeka. Hii ni kwasababu licha ya filamu za kiswahili kupendwa nchi mbalimbali lakini bado zinashindwa kufika huko hivyo wasambazaji wengine wakijitokeza ni rahisi kufika mbali na soko kukua maradufu na wasanii pia kufaidika katika mapato, na hili litakuwa na tija iwapo wasanii hawatauza haki zao zote kwa wasambazaji kupitia mikataba ya kinyonyaji, sheria pia zinatakiwa kuwekwa ili kumlinda mtengenezaji wa kazi husika katika kufaidika na kazi zake bila kusahau elimu kuhusu tasnia ya filamu.
                                             Baadhi ya wasanii wa filamu nchini

Like our facebook page Swahili World Planet for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.
Read More >>

Friday, July 5, 2013

Angalia Picha za utengenezaji wa filamu mpya 'Heart Attack' ya kajala










Hizi ni baadhi ya picha za msanii kajala Masanja katika utengenezaji wa filamu yake mpya ya heart attack itakayotoka kwenye mwezi wa kumi au kumi na moja.

Read More >>
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...