Nilisoma moja ya gazeti lililokua limeandikwa IGP atangaza dau la milioni 10 kwa yeyote atakaefichua wanaohusika na uvamizi wa kituo cha Polisi ambao pia walifanya mauaji ya Polisi wake wawili Bukombe Geita.
Baadhi ya mashuhuda wamekubali kuzungumza na akiwemo mlinzi ambae anafanya kazi eneo jirani na kituo hiki anaesema ‘Ilikua kitu kama saa tisa na dakika 40 niliona magari yanapitapita pamoja na pikipiki, kama muda wa dakika 5 nikasikia kitu kama tairi kimepasuka hisia yangu kwavile ni mlinzi mzoefu nilishtuka nikasema mbona hilo sio tairi manake gari sikuiona, kidogo tena nikasikia mengine yanapigwa kama mara tatu’
‘Vibunduki vidogo vikawa vinapigwa chapchap tu nikaanza kushangaa na kuanza kujifichaficha kukimbia huku na huku, ilipofika saa mbili tukakuta watu wawili wameuwawa Mwanamke mmoja na Mwanaume mmoja wametupwa kwenye mtaro barabarani, matukio kama haya yameshajitokeza mengi tu Geita mwingine amenyongwa tu barabarani lakini tuna muda mrefu hatukuyaona/kuyasikia’
Wakati tukisubiria ripoti nyingine ya Polisi kuhusu hili tukio unaweza kuwasikiliza mashuhuda wenyewe hapa chini.
Chanzo: millardayo.com