Baadhi
ya waandishi wa habari wakiwasikiliza wawasilishaji toka Wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo
Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Frank Mvungi)
Na Frank Mvungi
Serikali
imejizatiti katika kutekeleza mpango wa majaribio wa marekebisho ya
tabia kwa watoto walio katika mkinzano na sheria na walio katika hatari
ya kukinzana na sheria katika jamii.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu toka
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii bw. Steven Gumbo wakati wa mkutano na
waandishi wa habari.
“Serikali imefanikiwa kukamilisha kanuni za mahabusu za watoto, makao ya watoto na shule ya maadilisho” alisema Gumbo.
Pia hatua nyingine ni kukamilika kwa miongozo ya utoaji wa huduma katika mahabusu za watoto na shule ya maadilisho.
Hatua
nyingine ni kuwepo kwa mwongozo wa kijamiii (CRP) wa Marekebisho ya
tabia kwa watoto walio katika mkinzano na sheria na walio katika hatari
ya kukinzana na sheria.
Mafanikio
mengine ni kuwajengea uwezo watumishi wote wa mahabusi za watoto na
shule ya maadilisho juu miongozo mbalimbali iliyotolewa ya kuboresha
huduma katika Taasisi hizo.
Akieleza
zaidi Gumbo amesema kwa mujibu wa sheria ya mtoto, wanaokinzana na
sheria na ambao hawajapata dhamana kutoka katika mahakama wanapaswa
kupelekwa katika mahabusi za watoto, pale ambapo mahakama imejiridhisha
kuwa mtoto huyo ametenda kosa huamuru apelekwe katika shule ya
maadilisho.
Wizara
ya Afya kupitia idara ya Ustawi wa jamii imekuwa ikishirikiana na wadau
mblimbali kama vile Polisi, Mahakama, Magereza, Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora pamoja na mashirika mbalimbali ya Kitaifa na
Kimataifa katika kufanikisha na kutekeleza majukumu yake.
Watoto
wanaokinzana na sheria wanatunzwa katika mahabusi tano za watoto
zilizopo katika mikoa ya Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya na Dar es
salaam na katika shule ya maadilisho ya Irambo-Mbeya.