Hapo ni abiria wa Basi hilo la Taqwa wakisubiria Masaada ili waendelee na safari yao.
|
Muonekano wa Basi la Kampuni ya Taqwa baada ya kupata ajali na Watu
11 wamejeruhiwa vibaya baada ya basi hilo walilokuwa wakisafiria kutoa
Jijini Dar es Salaam kwenda Lubambashi nchini Congo DRC kugongana uso
kwa uso na lori aina ya Center wilayani Mbarali.
|
Watu
11 wamejeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya Taqwa walilokuwa
wakisafiria kutoa Jijini Dar es Salaam kwenda Lubambashi nchini Congo
DRC kugongana uso kwa uso na lori aina ya Center wilayani Mbarali.
Ajali
hiyo mbaya ilitokea juzi majira ya saa 2:00 usiku katika mtelemko wa
mlima Mambi katika barabara Kuu ya Mbeya –Iringa wilayani Mbarali
ikihusisha basi la Kampni ya Taqwa lenye namba za usajili T 396 AXZ na
lori aina ya Center lenye namba za usajili T 175 BRA.
Baadhi
ya watu walikuwa ndani ya basi hilo walisema kuwa wakati basi hilo
likiwa kwenye mwendo mkali katika mteremko huo, lori aina ya Center
ambalo lilikuwa likipandisha lilijaribu kupita gari lingine lilikuwa
limesimama kando ya barabara, ndipo magari hayo yalipogongana uso kwa
uso na kusababisha basi hilo kupoteza mwelekeo na kupinduka mtaroni.
Getruda
Kambale ambaye ni raia wa Congo, ni miongoni mwa abiria walionusurika
kwenye ajali hiyo ambaye alisema kuwa licha ya basi lao kubondeka
vibaya, hakuna mtu aliyepoteza maisha ingawa baadhi ya abiria wameumia
vibaya.
“Tunashukuru
Mungu hakuna mtu amekufa hapa, lakini dereva wetu ameumia vibaya
wamemchukua na kumkimbiza Hospitali,” alisema Kambale.
Alisema
wakati yeye akiwa amewa amechoka baada ya kusafiri kwa siku mbili
akitokea Nairobi, alishtikia basi likiyumba kasha akasikia kishindo
kikubwa na ndipo alijikuta akitolewa kwenye gari hilo kupitia dirishani.
Daktari
Msaidizi wa Hospitali ya Misheni Chimala, Peter Seif Kigombola alisema
kuwa hospitali hiyo imepokea majeruhi 11, kati yao 10 walikuwa ji abiria
wa basi la Taqwa na mmoja alikuwa ni dereva wa lori aina ya Center.
Alisema
abiria hao tisa hali zao zinaendelea vizuri, lakini wawili ambao ni
dereva wa basin a kondakta wake hali zao ni mbaya na kuwa wamepewa rufaa
ya kwenda katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa matibabu zaidi.
Alisema
kuwa dereva na kondakta wake walivunjika viungo mbalimbali vya miili
yao kama vile mikono na miguu na kupata majeraha mengine kichwani, hali
ambayo imesababisha hali zao kuwa mbaya.
Kaimu
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Barakael Masaki amethibitisha
kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa bado Jeshi la Polisi linaendelea
na uchunguzi wa ajali hiyo pamoja na kukusanya taarifa za majeruhi na
kuwa atatoa taarifa ya ajali hiyo baadaye.