Mwenyekiti wa CCM kata hiyo, Mudhihil Shoo akimsikiliza Diwani wa viti maalum Nuru Majitaka wakati akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Na Juma Mtanda,
Morogoro.
JUMUIYA ya wanawake
wa CCM Tanzania kata ya Sabasaba inatarajia
kupata kiasi cha Sh 7.9milioni kwa mwaka mara baada ya kuanzisha kwa miradi mbalimbali
yenye lengo la kuwainua akinamama na kujikwamua kiuchumi mkoani Morogoro.
Akizungumza na viongozi
wa Umoja wa wanawake Tanzania kata ya Sabasaba Manispaa ya Morogoro Mweny
ekiti
wa CCM kata hiyo mjini hapa, Mudhihir Shoo alisema kuwa endapo umoja huo
utajipanga vizuri kwa kusimamia miradi ya akinamama ya kujikwamua na kiuchumi
itasaidia kupata faida kiasi cha Sh4.3milioni mara baada ya kupata kiasi cha
Sh7.9 milioni kwa mwaka.
Shoo alisema kuwa
kazi iliyopo mbele yao ni namna ya kusimamia miradi hiyo baada ya kuanzishwa
kwake na wakifanikiwa kusimamia vema miradi hiyo italeta tija hasa kwa umoja
huo kuondokana na umasikini ndani ya chama na wanaumoja kwani nina imani
itasaidia upatikanaji wa ajira.
“Nimeona mchanganua
wetu wa miaradi yenu lakini cha msingi ni kujipanga namna ya kusimamia miradi
hiyo na nimeona kama mtaenda vizuri mnatarajia kupata Sh7,950,000milioni kwa
mwaka na faida halisi ni kiasi cha Sh3,620,000milioni mara baada ya kuanzisha
miradi yenu lakini itasaidia pia upatikanaji wa ajira” alisema Shoo.
Miradi hiyo ni
pamoja na ufugaji wa kuku wa kienyeji, utengenezaji wa batiki, sabuni na
uanzishaji wa benki za ushirika vijijini (VIKOBA) Tanzania ambapo kuanzishwa
kwa miradi hiyo inahitajika kiasi cha Sh4,324,000milioni kutokana na mali ghafi
mbalimbali.
Naye Diwani wa viti
maalumu kupitia tiketi ya CCM, Nuru Majitaka alisema kuwa Umoja huo unakabiliwa
na changamoto mbalimbali mojawapo ni upatikanaji wa fedha za uanzishwaji wa
miradi hiyo ambapo kiasi cha Sh4.3milioni ili kuweza kuanza kazi ya uzalishaji.
Majitaka alisema
kuwa tayari wanachama wametoa michango kiasi cha Sh98,000 ambapo ghalama za
kuanzisha miradi ni Sh4,226,000 na kuomba wadau mbalimbali wakiwemo marafiki wa
CCM, wafanyabiashara ndani na nje ya kata hiyo kujitokeza kuwasaidia ili
akinamama waondokane na tegemezi ndani ya chama na mtu moja moja.
Lengo kuu la mpango
huo ni kumwezesha mwanamke kuondokana na maisha duni, tegemezi na umasikini ili
kujitegemea na kuondokana na umasikini.