Kuhusu maamuzi ya kikao cha kamati kuu iliyoketi Dar es salaam July 6 -7 2013, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amesema mbali na kuainisha mapendekezo yanayostahili kuboreshwa, wamezikataa taarifa na kuzikanusha kwamba wamemtaka mmoja wa wajumbe ambae ni mwanachama wao Profesa Mwesiga Baregu kujiondoa ndani ya tume ya mabadiliko ya katiba.
Namkariri Freeman Mbowe akisema “tumeona mambo mengi yenye maslahi ya taifa, bado tumeona kuna mambo yanakwaza haki na demokrasia katika taifa ila hayo yote tusingependa kuchanganya na haya matukio mengine ya unyama…. hayo yote tutayatolea msimamo pamoja na vitabu na nini Chadema tunakwenda kufanya kwa nchi nzima kuhusiana na mchakato wa katiba”